Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, leo ataongoza Misa ya mkesha mwa Mwaka mpya, katika Kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga.
Kwa mujibu wa Katibu wa Askofu Padre Deusdedith Kisumo , Misa hiyo itaanza saa 4:00 usiku ambayo ni kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa mema ambayo ameyafanya kwa mwaka 2022 na kuomba baraka kwa mwaka mpya wa 2023.
Kesho Jumapili, Askofu Sangu pia ataongoza Misa ya Mwaka mpya katika kanisa hilohilo mabayo itakwenda pamoja na kufunga nadhiri za kwaza kwa watawa 6 wa Shirika la kijimbo la Mtakatifu Bikra Maria Mama mwenye huruma, na wengine wawili wa shirika hilo watafunga nadhiri za daima.
Misa ya Mwaka Mpya imepangwa kuanza saa 3:00 asubuhi