CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA KIGOMA(KGPC)CHAPITISHA MAAZIMIO

 

Rais wa umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC)Deogratius Nsokolo akifungua mkutano mkuu maalum kwa wanachama wa chama cha waandishi wa habari Mkoa Mkoa wa Kigoma(KGPC)

Na Editha Karlo,Matukio DaimaAPP,Kigoma

CHAMA cha waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma(KGPC)Kimefanya mkutano mkuu maalum,ambapo umepitisha maazimio kadhaaa yenye lengo la kuboresha hali ya utendaji kazi kutoka mafanikio yaliyopo sasa na kuwa bora zaidi.


Akiongea wakati akifungua mkutano huo Rais wa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania ambaye ni mwenyekiti wa  Kigoma press Club(KGPC)Deogratis Nsokolo alisema kuwa muungano wa vilabu vya habari Tanzania(UTPC)unakwenda kufanya mabadiliko makubwa katika kuvijengea uwezo vilabu vya habari nchini ili kuwa na mikakati ya kujiimarisha na kujiendeleza.


‘’Sasa hivi kila club ya waandishi nchini itatakiwa kuwa na mradi ambao utasaidia kuimarisha club hiyo ili hata wafadhili wetu watakaposuasua kutoa ruzuku au kujiondoa basi vilabu viwe na uwezo wa kujiendesha bila kuyumba kupitia miradi yao”alisema.


Nsokolo alisema kuwa sasa hivi UTPC watatoa pesa kwa klabu kulingana na mahitaji yake hivyo ni lazima klabu iombe fedha kwa mahitaji halisi ya klabu yake na bajeti hiyo itapitishwa na UTPC,pia klabu itapewa fedha kulingana na idadi ya wanachama wake.


Katika hatua ya kujiimarisha kwa KGPC kuna miradi mbalimbali ambayo mkutano mkuu imependekeza na kuwekwa chini ya kamati ya miradi kwa uchambuzi ili hatua za utekelezaji wa miradi hiyo uanze.


Nsokolo alisema Mkurugenzi mkuu wa UTPC Keneth Simbaya amehaidi kutembelea klabu ya Kigoma mwakani ili kujionea shughuli za maendeleo kwenye tasnia ya habari kwenye klabu hiyo.



Baadhi ya wanachama wa KGPC wakichangia kuhusu maazimio hayo waliwapongeza wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa UTPC kwa kuleta maazimio yenye kuzifanya klabu ziwe na misingi imara hasa katika usimamizi wa fedha.


Walisema baadhi ya klabu zimekuwa na migogoro hali lakini kwenye maazimio ya mkutano mkuu wa UTPC kuna wameweka mwongozo maalum wa utatuzi wa migogoro katika klabu.


‘’Haya maazimo ni mazuri na ndo maana tumeyapitisha tunachotakiwa kuyafanyia kazi kwaajili ya kuimarisha na kuendeleza klabu zetu”alisema mwanachama Prosper Kwigize


Naye katibu Mkuu wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma(KGPC)Mwajabu Hoza aliwasisitiza wanachama wote kulipa ada zao kwa wakati kila mwaka ambayo ni mapato ya msingi na hadi kufikia February 28 2023 mwanachama yeyote atakaye kuwa na deni atafukuzwa uanachama na hii ni kwa mujibu wa katiba.

Previous Post Next Post