Diwani wa kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
mheshimiwa Zamda Shaban amefanya mkutano wa hadhara uliolenga kutoa taarifa za
shughuli za maendeleo pamoja na kusikiliza changamoto zinazokwamisha maendeleo
katika kata hiyo.
Mkutano huo umefanyika kwenye uwanja uliopo mtaa wa
Mlepa kata ya Ndala ambapo wadau na viongozi mbalimbali wa mkoa, wilaya na
ngazi ya kata wamehudhuria kwa ajili ya kupokea na kutolea ufafanuzi kero za
wananchi.
Katika mkutano huo Wakazi wa kata ya Ndala wakiwemo
wazazi na walezi wametakiwa kushirikiana kwa pamoja kuondoa changamoto
zinazoikabili kata hiyo ikiwemo changamoto zilizopo kwenye shule ya msingi
Msufini pamoja na Ndala sekondari ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Hayo yameelezwa na walimu wa shule hizo katika
mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa kata ya Ndala Manispaa ya
Shinyanga Zamda Shaban kwa lengo la kutoa taarifa za shughuli za maendeleo na
kusikiliza changamoto zinazoikabili kata hiyo.
Mariam Salungi ni mwalimu wa shule ya msingi Msufini
pamoja na makamu mkuu wa shule ya sekondari Ndala Alphonce Deya wameeleza
changamoto huku wakiomba ushirikiano wa pamoja kwa wananchi ili kutatua
changamoto hizo.
Shule ya msingi Msufini inakabiliwa na changamoto ya
walimu ambapo idadi ya walimu katika shule hiyo ni 11 huku zaidi ya wanafunzi elfu moja mianane ishiringi wanaendelea na
masomo.
Mwalimu Mariam Salungi amesema hali hiyo inachangia
wanafunzi wengi kutofaulu na shindwa kuendelea
na masomo ya kidato cha kwanza
Akizungumza diwani wa kata ya Ndala Zamda Shaban
ameendelea kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Luluhu
Hassan kwa kuleta fedha za maendeleo katika kata ya Ndala ambapo amesema hakuna
changamoto iliyokwamisha miradi hiyo.
Mheshimiwa Zamda jina maarufu Tausi amewaomba wazazi na wananchi kwa ujumla wa kata
ya Ndala kuendelea kushirikiana katika
shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Niwaombe
wazazi tushirikiane na walimu ili shule iendelee kufanya vizuri shule ya msingi
Msufini bado ni tatizo Mwaka huu wamefeli watoto 50 kwa umliwalionao wataenda
wapi na watafanya kazi gani hawa bado watoto wadogo sana Watoto 50 kwenye kata
yetu ni wengi sana lakini ni kwa sababu ya miundombinu mibovu na hili swala
tulishalileta kwenu angalau tuweze kupata shule ya awali Msufini B”.amesema
Diwani Zamda
“Pamoja
na jitihada zote za serikali isiwe sababu ya sisi wananchi kuacha kuchangia
maendeleo ya watoto wetu tutakapoanzisha boma letu serikali itakuja kutuunga
mkono na walimu tutaletewa wapya kwahiyo niwaombe sana wazazi na wananchi wa
kata ya Ndala tushirikiane kwa pamoja kuondoa changamoto hii ya watoto wetu”.amesema
Diwani Zamda
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Manispaa ya
Shinyanga, mratibu wa TASAF Manispaa hiyo Octavina Kiwone naye amewasisitiza
wananchi wa kaya ya Ndala kuwa na utaratibu wa kuungana kwa pamoja katika
utatuzi wa changamoto shughuli ya kuboresha miundombini.
Mkutano huo wa hadhara ambao uliandaliwa na Diwani
wa kata ya Ndala Zamda Shaban kwa ajili ya kutoa taarifa za shughuli za
maendeleo na kusikiliza kero za wananchi huku akiahidi kuendelea na utaratibu huo
kila baada ya mienzi mitatu ambapo wananchi wamepata nafasi ya kuuliza maswali
juu ya changamoto zinazowakabili.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Ndala wameonekana kutolidhishwi
na huduma zinazotolewa na shirika la umeme Mkoa wa Shinyanga pamoja na huduma
za bima ya Afya katika kituo cha afya Kambarage.
Wananchi hao wameeleza kuwa bado hawalidhishwi na
huduma zinazotolewa na TANESCO Mkoa wa Shinyanga huku huduma za CHF zikitajwa
kuwa ni changamoto kwa baadhi ya wananchi.
Moja ya changamoto zilizotajwa ni wananchi wanaoomba
kuunganishiwa umeme wengi hushindwa kupata kwa wakati na wengine kutopata
kabisa hali ambayo inaendelea kurudisha nyuma maendeleo ya baadhi ya wakazi wa
kata ya Ndala.
Kaimu meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Kurwa Mangara ameahidi kushughulikia changamoto zote zilizowasilishwa na wananchi
kupitia mkutano huo wa hadhara.
Naye mganga
mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert ameeleza juu ya huduma za bima
ya afya katika kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga ambapo amesema kituo
hicho kinatoa huduma nyingi za bure hali inayochangia dawa zinazolewa kuisha
mapema.
Aidha mtendaji wa kata ya Ndala Joshua Masengwa
wakati akisoma taarifa fupi ya shughuli za maendeleo kwa robo 2 ya Mwaka wa
fedha 2022\2023 kuanzia Septemba hadi Desemba 2022, amesema kwa sasa kata hiyo
inakituo kimoja cha afya cha mtu binafsi ambacho kinahudumia wananchi.
“Kwa
sasa kata ya Ndala inakituo kimoja cha afya cha binafsi ambacho kinahudumia
wananchi kiitwacho Inspire lakini pia wananchi wameendelea na huduma za afya
kupitia kituo cha afya cha Kambarage pamoja na Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga”.
“Moja
ya mpango mkuu kwa Mwaka huu wa fedha ni kuanza kujenga kituo cha afya katika
eneo la mtaa wa Mlepa ambalo kwa sasa liko chini ya ofisi ya mkurugenzi wa
Manispaa baada ya wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo kuliptwa fidia”.amesema
Mtendaji Masengwa
Diwani wa kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga mh:
Zamda Shaban amefanya mkutano wa hadhara Desemba 30,2022 kwa lengo la kutoa
taarifa za shughuli za maendeleo na kusikiliza kero za wananchi mkutano huo
umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo wakuu wa idara katika
Manispaa ya Shinyanga.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Ndala wamempongeza
Diwani huyo Zamda Shaban kwa kuendelea na utaratibu wa kufanya mkutano
kusikiliza kero zao kila baada ya mienzi mitatu ambapo wamesema hali hiyo
inawasaidia kupata ufumbuzi zaidi juu ya changamoto zilizopo.
Diwani wa kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Zamda Shaban akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara.
Mwakilishi wa mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, mratibu wa TASAF Manispaa hiyo Octavina Kiwone akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwakilishi wa mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, mratibu wa TASAF Manispaa hiyo Octavina Kiwone akizungumza kwenye mkutano huo.
mtendaji wa kata ya Ndala Joshua Masengwa akizungumza katika mkutano huo wa hadhara.
Mwalimu wa shule ya msingi Msufini Mariam Salungi akieleza changamoto zinazokwamisha maendeleo kitaaluma shuleni hapo.
makamu mkuu wa shule ya sekondari Ndala Alphonce Deya
akieleza mafanikio na changamoto zilizopo katika shule ya sekondari Ndala.Mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert
akijibu maswali katika mkutano wa hadhara kata ya Ndala.Kaimu meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga K
urwa Mangara akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wananchi katika mkutano wa hadhara kata ya Ndala.Mkazi wa kata ya Ndala akiuliza maswali kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa kata ya Ndala mheshimiwa Zamda Shaban.Mkazi wa kata ya Ndala akiuliza maswali kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa kata ya Ndala mheshimiwa Zamda Shaban.Mkazi wa kata ya Ndala akiuliza maswali kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa kata ya Ndala mheshimiwa Zamda Shaban.Mkazi wa kata ya Ndala akiuliza maswali kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa kata ya Ndala mheshimiwa Zamda Shaban.Mkazi wa kata ya Ndala akiuliza maswali kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa kata ya Ndala mheshimiwa Zamda Shaban.Mkazi wa kata ya Ndala akiuliza maswali kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa kata ya Ndala mheshimiwa Zamda Shaban.Mkutano wa hadhara ukiendelea katika kata ya Ndala ambao umeandaliwa na Diwani wa kata hiyo Zamda Shaban.Mkutano wa hadhara ukiendelea katika kata ya Ndala ambao umeandaliwa na Diwani wa kata hiyo Zamda Shaban.