Ticker

6/recent/ticker-posts

IDADI YA WATOTO WALIOZALIWA KATIKA MKESHA WA KRISMASI SHINYANGA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jumla ya watoto 11 wamezaliwa katika mkesha wa krismass katika kituo cha Afya cha kambarage katika Manispaa ya Shinyanga,  kati yao wakike ni 4 na wakiume 7 wote wakiwa na afya njema

Misalaba Blog imetembelea na kuzungumza na muuguzi wa Wodi ya wazazi katika kituo cha afya Kambarage Onesmo Godwin Mwamafupa ambaye  amesema  kuwa  jumla ya watoto  hao 11 wamezaliwa katika mkesha wa kristmass katika kituo hicho.

Mwamafupa ameeleza kuwa  watoto hao wamezaliwa wakiwa na uzito wa kawaida na kwamba hakuna changamoto juu yao.

Aidha Misalaba Blog pia imefika katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambapo Muuguzi  wa Wodi ya wazazi Mariam Abdallah ameeleza kuwa hakuna Mtoto aliyezaliwa katika mkesha wa sikukuu ya krismasi.  

                                 

kuzungumza na muuguzi wa Wodi ya wazazi katika kituo cha afya Kambarage Onesmo Godwin Mwamafupa akizungumza na Misalaba Blog.


Post a Comment

0 Comments