Katika kuelekea
Sikukuu za Mwisho wa Mwaka Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limepiga marufuku
Disco toto katika kusherehea Sikukuu ya Mwaka Mpya na Christmas huku likitoa
wito kwa Wazazi na Walezi kuhakikisha watoto awaendi kwenye madisco ambayo
yanaweza kuleta msongano na kusababisha madhara kwa watoto.
Agizo hilo limetolewa
na Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Mwanza Kamishina Mwandamizi Msaidizi Wilbroad
Mutafungwa wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo.
Aidha Jeshi la Polisi
Mkoani Mwanza linawataka watumiaji wote wa barabara ikiwa ni watembea kwa
miguu,wapanda baiskeli,wasukuma guta na wanaotumia vyombo vya moto kila mmoja
kwa nafasi yake ahakikishe anafuata sheria za usalama barabarani ili kuweza
kuzuiabajali zinazoweza kuepukika
Katika hatua Nyingine Kamanda Mutafungwa ameitaka jamii ibadilike na kuachana na dhana potofu iliyojengeka kwa mwisho wa mwaka huwa na matukio mabaya yakihusisha vifo,uhalifu ,mikosi na ajali za barabarani badala yake wachukulie kawaida na waamini kuwa ni kipindi kama vikivyo vipindi vingine na waishi kwa kufuata sheria .