Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kuelekea msimu wa sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya Jeshi
la Polisi Mkoa wa Shinyanga limepiga marufuku kuwepo kwa Disko toto huku likiagiza
kufungwa kwa Bar zote baada ya saa sita usiku, isipokuwa zile zenye vibali
maalum.
Akizungumzia hali ya ulinzi na usalama wakati wa
sherehe za krismasi na Mwaka mpya Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga
Janeth Magomi amewataka wazazi na walezi kuwajibikia jukumu la kuwasimamia
vyema watoto katika kipindi hicho cha sikukuu.
Kamanda Magomi amesema baada ya saa sita usiku bar
zote zitafungwa isipokuwa zitakazoendelea kutoa huduma ni zile zenye vibali
maalum.
“Disko
toto zimepiga marufuku na tutakwenda kwenye kumbi zote kuhakikisha kuwa hakuna
disko toto na niwatake wazazi kuendelea kuwasimamia hawa watoto tusherehekee
hizi sikukuu kwa amani na utulivu majumbani kwetu lakini siyo kuwapeleka kwenye
disko toto watoto wetu”amesema
ACP Magomi
“Niwatake
wazazi tusimamie watoto wetu sambamba na hilo sisi jeshi la polisi tumejipanga
vizuri kusimamia sheria kwa maana ya kusimamia doria, misako na oparesheni
mbalimbali kwahiyo walevi sheria iko wazi mwisho wa kunywa pombe unajulikana
baada ya saa sita Bar zote zifungwe
labda kwa zile ambazo zinavibali ndiyo wanaweza kuendelea sisi
tutaendelea kusimalia hayo na wale wote ambao tutawabaini tutakamata na kuwafikisha
kwenye vyombo vya sheria”.amesema
ACP Magomi
Kamanda Magomi amesema jeshi hilo limejipanga vizuri
kuhakikisha wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga wanasherekea sikukuu za Krismas
na Mwaka mpya kwa amani na utulivu ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi kwenye
nyumba za ibada.
“Jeshi
la Polisi tumejipanga vizuri kwenye ibada tutakuwepo kwa maana ya kuhakikisha
ulinzi wa kila raia upo vizuri lakini pia tumejipanga vizuri kwa maana ya
barabarani kwenye mitaa na sehemu zote za starehe kuhakikisha kuwa hizi sikukuu
zinapita kwa hali ya usalama kabisa”.amesema
Kamanda Magomi