KIKUNDI CHA BINTI SHUJAA WAFANYA SHEREHE - DIWANI WA MASENGWA SHINYANGA- MWANAMKE FANYA UJASILIAMALI

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jamii hasa kundi la vijana wametakiwa kujishughulisha na biashara ama kazi mbalimbali za kuwaingizia kipato kwa kuwanufaisha wao, jamii na Taifa kwa ujumla ili kuondokana na hali tegemezi ya kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa kata ya Masengwa Mh:Nikodemus Luhende Simon kwenye sherehe ya kikundi cha Binti shujaa iliyofanyikia kijiji cha Bubale kata ya Masengwa Halmashauri ya Shinyanga vijijini.

Diwani Nikodemus amekipongeza kikundi hicho huku akiwasisitiza wanawake hasa kundi la vijana kufanya kazi kwa bidii ili kuepuka wimbi la ugumu wa maisha linalochangia baadhi ya wasichana kupoteza maadili yao.

“ Mama Dkt. Samia anasema tunataka tuwe na Taifa linalojitegemea kiuchumi ile ya Mwanamke kumtegemea Baba hiyo imeshapitwa na wakati mwanamke wa sasa kama unauwezo wa kubeba michicha, unauwezo wa kubeba Nyanya, unauwezo wa kubeba Dagaa fanya hivyo tunataka tuondokana na Taifa tegemezi la kuwategemea hawa wababa”.amesema Diwani Nikodemus

“Ombi langu kwa mabinti wengine na vikundi vingine  tujifunzeni ujasiliamali Dunia inaelekea huko Mama Dkt. Samia anasema katika Dunia tunayoishi ni hamsini kwa hamsini kwahiyo mama anataka sisi wote tuwe levo moja kwahiyo mnatakiwa mpambane kama hamtapambana tena, mfanye kazi kama hamtafanya tena tusije tukaingia kwenye lile wimbi la ombaomba kwa sababu ya ugumu wa maisha”.amesema Mh: Simon

“Kwa maana hiyo sasa mimi niwaomba watu wa binti shujaa fanyeni kazi bila uoga msikatishwe tamaa na mtu”.amesema Diwani Simon

Kikundi cha Binti shujaa kipo chini ya shirika la Rafiki SDO ambapo wawezeshaji kutoka shirika hilo wameeleza juu ya kikundi hicho na kwamba ni utekelezaji wa mradi wa Epic unaolenga kupunguza maambukizi mapya ya UKIMWI kwa mabinti balehe na wanawake vijana.

Wamesema wataendelea na uwezeshaji huo ili kuwaimarisha wanawake hasa wasichana waweze kuepukana na mambo yasiyofaa katika jamii kwa manufaa ya Taifa.

Awali katika risala ya kikundi cha Binti shujaa iliyosomwa na Maria Mahona wameeleza changamoto zilizopo ikiwemo kukosa  ujuzi zaidi katika mambo ya ujasiliamali ili kukusa michati yao na kuinuka kiuchumi ikiwa lengo lao ni kuondokana na maisha tegemezi.

Misalaba Blog imezungumza na baadhi ya wanakikundi wa Binti Shujaa ambao wameahidi mabadiliko chanya baada ya hatua hiyo.

Kikundi cha Binti Shujaa kiliundwa Desemba 20,2021 kwa ajili ya kuweka akiba na kukopa ambapo Desemba 2022,  wamefikia siku ya kugawana fedha zao hafla ambayo imehudhuriwa na wadau pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Diwani viti maalum kata ya Masengwa Bi. Suzana Malembela.

Vikundi vingine ambavyo vimehudhuria sherehe hiyo ni pamoja na kikundi cha Amani na kikundi cha Nguvu kazi.

Diwani wa kata ya Masengwa Mh:Nikodemus Luhende Simon akizungumza kwenye sherehe ya kikundi cha Binti Shujaa Bubale.

Maria Mahona akisoma 

risala ya kikundi cha Binti shujaa

.







TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Previous Post Next Post