RAIS DKT.SAMIA ATOA ZAWADI ZA KRISMASI KWA WATOTO YATIMA KATAVI

 

Na: Zillipa Joseph, Katavi.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe.Jamila Yusuph Kimaro kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko  amekabidhi zawadi mbalimbali za Krismasi  zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kituo cha kulelea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu cha Mt.Yohane Paul wa pili kilichopo Mjini Mpanda Mkoani Katavi.
Zawadi zilizokabidhiwa kutoka kwa Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kituoni hapo  ni pamoja na Kilo Hamsini za Mchele, Mbuzi wawili, Maharage Kilo Hamsini, Lita Ishirini za Mafuta ya kupikia, pamoja na vitu vingine.
Akizungumza kwa niaba ya Mhe.Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,amemshukuru Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa msaada alioutoa kwa watoto hao yatima  ambapo ametoa wito kwa Jamii Nchini kuwakumbuka watu walio katika makundi maalumu.
Kwa Upande wake Mkuu wa Kituo hicho Sista Rozi Sungura amemshukuru Rais Dkt.Samia pamoja na uongozi wa Mkoa kwa kuona umuhimu wa kutoa msaada huo kwa watoto hao na ametoa wito kwa Jamii kujumuika kuiga Mfano wa viongozi kujumuka na watoto hao kwa kuwasaidia katika mahitaji mbalimbali.
Previous Post Next Post