RIDHIWANI-SERIKALI INAENDELEA KUVALIA NJUGA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI

 


Na Mwandishi wetu..
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais dkt.Samia Suluhu Hassan inaendelea kusimamia utatuzi wa migogoro mbalimbali ya ardhi ili kulinda Amani, Usalama  na Utulivu ndani ya jamii.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete alipofanya ziara ya Kikazi Wilayani Same. 
Akiongea na wananchi aliwaahidi kuwa migogoro yote inatambulika na hivyo serikali inapambana kutatua ili kurejesha Amani katika maisha ya Watanzania. 
Katika siku hii Ridhiwani pia alishiriki Fainali ya Michezo ya kombe la Mbunge Anne Kilango ambapo Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela nae alishiriki. 
Previous Post Next Post