Ticker

6/recent/ticker-posts

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TCRA JUU YA LESENI


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa chini ya Sheria  ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na.12 ya 2003, na kupewa jukumu la kusimamia Sekta  ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta nchini Tanzania. 

TCRA imebaini kuwepo kwa makampuni na watu binafsi wanaofanya biashara ya kutoa  huduma za televisheni kupitia satelaiti bila kuwa na leseni halali pamoja na uingizaji wa vifaa  vya mawasiliano, ikijumuisha visimbuzi vya Canal Plus na vifaa vingine vinavyofanana na  hivyo ambavyo havijaidhinishwa na TCRA. 

Kwa mujibu wa Kifungu cha 23 (1) (b) na (c) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na  Posta iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022, ikisomwa pamoja na kanuni ya 40 (a) ya Kanuni za  Leseni za 2018 zinaelekeza wasambazaji wa vifaa vya kieletroniki kuwa na leseni. Pia kifungu  cha 83(1) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kinaelezea umuhimu wa vifaa  vya kieletroniki vinavyoingia nchini kuidhinishwa na TCRA kabla havijaanza kutumika. 

TCRA, inautaarifu Umma na wafanyabiashara wote wanaofanya biashara ya huduma za  televisheni kupitia satelaiti bila kuwa na leseni halali pamoja na wanaoingiza nchini vifaa vya  mawasiliano, ikijumuisha visimbuzi vya Canal Plus na vifaa vingine vinavyofanana na hivyo  ambavyo havijaidhinishwa na TCRA kuacha mara moja kufanya hivyo na badala yake kufuata  utaratibu wa kupata leseni. 

Kwa atakayeshindwa kutekeleza ilani hii, TCRA itachukua hatua za kisheria na za kiudhibiti bila kutoa taarifa nyingine. 

IMETOLEWA NA 

MKURUGENZI MKUU 

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA 

30 Desemba 2022

Post a Comment

0 Comments