VIONGOZI SHINYANGA WATUMA SALAMU ZA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2023

 

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wakati tukielekea Mwishoni mwa Mwaka 2022 wadau mbalimbali Mkoani Shinyanga wameipongeza  redio faraja katika kukuza na  kuchochea Maendeleo ya Mkoa na Taifa

Wamesema kupitia vipindi na Taarifa za habari mbalimbali kituo cha redio faraja kimekuwa chachu ya kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya muhimu,lakini pia kuhamasisha uwajibikaji wa mamlaka mbalimbali.

Katika salamu zake za Krismass na Mwaka Mpya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt Jomaari Satura licha ya kuwaomba wananchi kuendelea kudumisha amani lakini amewataka kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kilimo chenye tija ili kuendelea kukuza uchumi kupitia kilimo

Akitoa salamu za krismass na Mwaka Mpya Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga, Injinia Yusuph katopora amesema Mamlaka hiyo itaendelea kuwahudumia wananchi kwa ubora wa hali ya juu

 Naye Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa magereza Josephine Semwenda katika salamu zake za krismas na Mwaka mpya amewakumbusha wananchi kufanya tathimini ya malengo waliyokuwa wamejiwekea kwa Mwaka 2022,ikiwa ni pamoja na kuweka mipango kwa ajili ya Mwaka 2023

Previous Post Next Post