Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Angelo Accattino kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Tanzania.
Kabla ya uteuzi huo, Askofu mkuu Angelo Accattino alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Bolivia.
Askofu mkuu Angelo Accattino alizaliwa tarehe 31 Julai 1966, Jimboni Casale Monferrato, nchini Italia, ambapo baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre tarehe 25 Juni 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.
Askofu mkuu Angelo Accattino alianza utume wake katika masuala ya diplomasia ya Vatican, tarehe 1 Julai 1999.
Tangu wakati huo akatekeleza dhamana na utume wake huko Trinidad na Tobago, Colombia, Perù, Vatican na hatimaye, Marekani na Uturuki.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 12 Septemba 2017, akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Bolivia na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu ambapo aliwekwa wakfu kama Askofu mkuu tarehe 25 Novemba 2017.
Amebahatika kutunukiwa Shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa.
Leo tarehe 2 Januari 2023 ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Tanzania.
SOURCE:VATCAN NEWS, RADIO FARAJA