Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, imeendelea kuwa miongoni mwa halmashauri chache nchini zinazowakutanisha watumishi wa
kwa kufanya Bonanza.
Hali hiyo imejidhihirisha wakati wa Bonanza la michezo la watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kasulu lililofanyika kwenye viwanja vya chuo cha ualimu Kasulu.
Wakizungumza wakati wa Bonanza hilo, baadhi ya mashuhuda kutoka katika halmashauri jirani za Buhigwe na Mji wa Kasulu walioshuhudia hemwa hemwa zilizokuwepo kwenye viwanja hivyo, walionesha matanio ya kuwa na mabonanza katika halmashauri zao jambo ambalo halijawahi kufanyika.
"Tutafanya Bonanza na sisi mwaka huu mwenyezi mungu akitujaalia", alisikika mwalimu mmoja wa halmashauri ya Mji wa Kasulu aliyekiwepo kwenye Bonanza hilo kwa masharti ya jina lake kuhifadhiwa.
Katika Bonanza hilo jumla ya michezo 21 ilifanyika ikihusisha zaidi ya watumishi 100 wa halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wengi wao wakitoka katika idara za afya, elimu msingi, elimu sekondari, utawala na makao makuu ya halmashauri.
Bonanza hilo lililotanguliwa na tukio la Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Joseph Kashushura kushiriki katika mbio za kuzunguka uwanja, lilifuatiwa na michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, riadha, kuvuta kamba na kufukuza kuku.
Michezo mingine iliyoshuhudiwa wakati wa Bonanza hilo ni kukimbia kwenye magunia, kuruka juu na vipaji.
Akizungumza wakati wa hafla iliyoambatana na Bonanza hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Joseph kashushura amewashukuru watumishi wa halmashauri hiyo kwa ushiriki wao na kuwataka waendelee kuwa na umoja.
Amesema kuwa ataendelea kushughulikia kero mbalimbali na kuzitaja baadhi ya kero hizo kuwa ni pamoja na usafiri wa kurudi na kwenda kazini.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kutoa zawadi kwa washindi wa Bonanza hilo, Kashushura aliyekuwa mgeni resmi kwenye hafla hiyo, amewata watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kuzingatia misingi ya kazi itakayoiwezesha halmashauri hiyo kuwahudumia wananchi pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato.
"Tutaendelea kufanya mabonanza ya kutukutanisha na kwa kuboresha zaidi yatakuwa yakifanyika kila baada ya robo"amesema