CCM MKOA WA SHINYANGA WAMPONGEZA RAIS DKT. SAMIA KURUHUSU MIKUTANO VYAMA VYA SIASA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa  kwa kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ifanyike kwa kufuata kanuni na sheria za Nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 7,2023 katika ofisi za CCM Mkoa wa Shinyanga, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Mabala Mlolwa amesema kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini  ni kuendeleza demokrasia safi yenye kujenga na kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa watanzania na Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti Mh: Mlolwa amesema chama cha mapinduzi Mkoa wa Shinyanga kinaungana na wito wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kauli za maridhiano na maboresho mbalimbali kwenye vyama vya siasa na kwamba hatua hiyo inaleta chachu ya kisiasa kwa kushindana kwa hoja.

“CCM Mkoa wa Shinyanga tunamshukuru na kumpongeza sana Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nitoe hongera kubwa kwa mambo mengi anayoyafanya hususan hili la kupanua demokrasia katika Nchi yetu kuruhusu vyama rafiki kupanua wigo wa demokrasia na kuruhusu waweze kufanya mikutano yao ya kisiasa hili sisi  Mkoa wa Shinyanga tunampongeza sana na tunamshukuru sana Mama Dkt. Samia kwakweli amepanua demokrasia Nchini.amesema Mabala

“Rais Dkt. Samia kuruhusu mikutano kwa vyama vya siasa ifanyike  ameleta chachu ya kisiasa ambayo tutashindana sasa kwa hoja kwahiyo mkoa wa Shinyanga tumeyapokea kwa asilimia mia moja tutafanyakazi kwa kuhakikisha maelekezo ya Mwenyekiti wa chama Taifa yanatekelezwa”.amesema Mabala Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga

Wakati huo huo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye kugusa jamii na Mkoa wa Shinyanga miongoni mwa mikoa iliyonufaika na fedha za miradi  katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu pamoja na miundombinu.

Mheshimiwa Mlolwa wakati akimpongeza Rais Dkt. Samia amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Shinyanga  kuwa fedha zote za miradi zimetumika vizuri na kwamba hakuna ubadhirifu wowote juu ya miradi hiyo.

“Tangu uanzishwe Mkoa wa Shinyanga hatujawahi kupokea fedha nyingi na miradi mingi lakini chini ya Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa muda wa Mwaka mmoja na sehemu alioingia tumepokea fedha nyingi kweli na mabadiliko ya kimaendeleo yameonekana”. Amesema Mabala

“Kwenye sekta ya elimu tulianza na ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa Mkoa wa Shinyanga tumejengewa vyumba vya madarasa mia nne na viti vyake zikiwemo shule shikizi ambapo mwanza kabla ya Mama Samia wananchi wetu tulikuwa tunawachangisha lakini kwa huruma yake madarasa yamejengwa kuanzia hatua ya kwanza  mpaka yamekamilika bila mchango wa fedha ya mwananchi kwahiyo tunamshukuru sana Rais Samia”.

“Lakini pia Mkoa wa Shinyanga watoto wengi wa kike walikuwa wakikatisha masomo yao mara nyingi kwa kupata mimba mama Samia ameliona hili tayari alileta fedha na shule imeshakamilika ya watoto wa kike huyu mama Samia ni kiongozi wa mfano na tunapaswa kumuiga katika historia yake hiii nzuri kingine katika kipindi cha nyuma serikali ya awamu ya tano ilifuta ada ya elimu ya msingi lakini huyu Mama ameingia akafuta ada hadi kidato cha sita wanafunzi wanasoma bila kutoa ada shuleni”.

 

“tulifanikiwa kupata fedha za ujenzi wa vituo vya afya lakini pia tunamachinjio ya nyama na Mkoa wetu huu wa Shinyanga tunawafugaji wengi  wataendelea kunufaika na mradi huo na soko lake la nyama litakuwa kubwa lakini pia kuna mradi wa maji unaendelea Wilaya ya Kishapu ambako wananchi walikuwa wanateseka sana na Mama Samia aliliona hilo”.amesema Mabala

“Mkoa wa Shinyanga unajishughulisha na kilimo, ufugaji, madini pamoja na biashara tunaendelea kumshukuru Rais Dkt. Samia kwa kutengeneza mazingira rafiki ya shughuli zetu kuendelea vizuri ikiwa ni pamoja na kupokea mbolea na mbegu za pamba kwa wakati hivyo CCM Mkoa wa Shinyanga tunampongeza sana Rais Samia kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi ya Mwaka 2020 – 2025”. Amesema Bwana Mabala

“Tutaendelea kusimama Mama Samia  kwa mambo haya anayoyafanya ni dhahiri kwamba anatosha na sisi tupo tayari kumsaidia kwa kutimiza wajibu wetu kwenye chama na kujibu hoja za vyama vingine kwa hoja na tunawaomba vyama vingine  nao wajielekeze kwenye siasa za ajenda ili kukuza demokrasia yetu kwa maslahi mapana ya Taifa letu lakini pia ndiyo shabaha kuu ya maridhiano yetu yanayoendelea mpaka sasa”.amesema Mwenyekiti CCM Mkoa wa Shinyanga Mh: Mabala

 

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa ofisi za CCM Mkoa, kulia mwenye Tisheti ya njano ni Mwenyekiti wa umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Shinyanga Clement Osward Madinda






Previous Post Next Post