HAWA NDIYO WATOTO WALIOZALIWA TAREHE 1.1.2023 SHINYANGA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Jumla ya watoto 11 wamezaliwa katika mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya kwenye kituo cha Afya cha kambarage Mjini Shinyanga,  kati yao wakike ni 6 na wakiume 5 wote wakiwa na afya njema.

Misalaba Blog imetembelea na kuzungumza na muuguzi wa Wodi ya wazazi katika kituo cha afya Kambarage Hilda Mahemba ambaye ameeleza kuwa  watoto hao wamezaliwa wakiwa na uzito wa kawaida na kwamba hakuna changamoto juu yao.

Misalaba Blog  pia imefika katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga na kuzungumza na afisa muuguzi msaidizi wodi ya wazazi Experantia Misalaba ambaye ameeleza kuwa watoto watatu wamezaliwa katika mkesha wa sikukuu ya Mwaka mpya.

Kati ya watoto hao watatu wakike ni 2 na mmoja ni mototo wa kiume ambapo Muuguzi msaidizi Experantia Misalaba ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kwenda kupata huduma katika Hospitali hiyo pale mama aonapo dalili za ujauzito.

Baadhi ya akina mama waliojifungua katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga pamoja na kituo cha afya Kambarage wameshukuru kwa huduma nzuri walizopata na kwamba hakuna changamoto yoyote iliyotokea juu yao.

M

uuguzi wa Wodi ya wazazi katika kituo cha afya Kambarage Hilda Mahemba 

akitaja idadi ya watoto waliozaliwa usiku wa mkesha wa sikukuu ya Mwaka mpya 2023.



Previous Post Next Post