KWAYA YA BBC SHINYANGA YAZINDUA ALBAMU, Brother K NA MAMA NJELEKELA WACHEKESHA UKUMBINI LIVE

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

 Kwaya  inayojulikana kwa jina la Bonde la Baraka Choir (BBC) kutoka katika kanisa la International Evangelical Assemblies of God Tanzania (IEAGT) Kambi ya waebrania imezindua albamu mpya inayokwenda kwa jina la UZAO MTEULE Mkoani Shinyanga.

Uzinduzi huo umefanyika Mwezi huu Januari 1,2023 katika ukumbi wa Lyakale Hotel uliopo Manispaa ya Shinyanga hafla ambayo imehudhuriwa na wadau pamoja na viongozi mbalimbali kutoka taasisi za dini, sekta binafsi na viongozi kutoka Manispaa ya Shinyanga.

Mgeni rasmi katika halfa hiyo alikuwa Bwana Martin Ringi kutoka katika Kampuni ya Ringi Enterprises Mkoani Shinyanga ambapo pia hafla hiyo ilihudhuriwa na kikundi cha wachekeshaji FUTUHI kutoka Mkoa wa Mwanza kikiongozwa na BROTHER K, a.k.a tajiri wa Kigoma.

Akisoma risala ya kwaya ya Bonde la Baraka (BBC) Elizabeth Stevin amesema uongozi wa kwaya hiyo utaendeleza jitihada madhubuti za kushirikiana na makanisa mengine katika kusambaza albamu ili kumhubiri Mungu kwa njia ya uimbaji.

Amesema mikakati ya kwaya ya BBC ni kuhakikisha injili inawafikia watu kwa kushirikiana na makanisa mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga.

 Bonde la Baraka choir (BBC) iliweka mpango wa kurekodi nyimbo sita za video kwa ajili ya kutangaza injili mpango ambao ulianza Julai Mwaka 2022 na kukamilika Desemba 2022 ambnapo albamu ya UZAO MTEULE imerekodiwa kwa kuchukua maudhui katika maeneo ya Mkoa wa Shinyanga.

Mipango wa kwaya hiyo ni kuwa na vyanzo vya mapato vya kuweza kujiendesha kiuchumi kwa ajili ya kugharamia shughuli za uendeshaji wa kwaya ambapo katika mipango hiyo ni pamoja na kununua mashine za kisasa za kufyatua matofali huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi katika kalenda za shughuli zao za Mwaka katika kupeleka ujumbe kwenye jamii hasa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika halfa hiyo Bwana Martin Ringi kutoka  Kampuni ya Ringi Enterprises ameipongeza kwaya ya BBC kwa nyumbo zao nzuri huku akiwasihi kutokata tamaa katika hatua kutangaza neno la Mungu kwa njia ya uimbaji.

Naye katibu wa kanisa la International Evangelical Assemblies of God Tanzania (IEAGT) Lucas Lugwila amewasisitiza wanakwaya kuendelea na juhudi za kumwimbia Mungu na kutoa ujumbe kwa jamii hasa ya Mkoa wa Shinyanga.

‘Uongozi wa kwaya ya BBC umejipanga kuwa na albamu nyingine ya video kwa Mwaka 2023 kwa ajili ya kutangaza injili ya Yesu kristo kwa watanzania ambapo alibamu ijayo itafanyiwa nje ya Mkoa wa Shinyanga kwa maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii lengo la kutangaza utalii wa Taifa la Tanzania kupitia injili’.

Mgeni rasmi katika halfa hiyo Bwana Martin Ringi kutoka  Kampuni ya Ringi Enterprises Mkoani Shinyanga akizungumza kwenye uzinduzi wa albamu ya UZAO MTEULE kwaya ya BBC kutoka Shinyanga.

katibu wa kanisa la International Evangelical Assemblies of God Tanzania (IEAGT) Lucas Lugwila akizungumza kwenye halfa ya uzinduzi wa albamu ya UZAO MTEULE kwaya ya Bonde la Baraka (BBC).

Akisoma risala ya kwaya ya Bonde la Baraka (BBC) Elizabeth Steven katika uzinduzi wa albamu yao inayokwenda kwa jina la UZAO MTEULE.







TAZAMA VIDEO YA BROTHER K WAKICHEKESHA NA MAMA NJELEKELA SHINYANGA
Previous Post Next Post