MCHUNGAJI LUGEMBE AWAKUMBUSHA WAKRISTO KUMSHUKURU MUNGU

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mchungaji msaidizi wa Askofu kanisa la Africa Inland Church Tanzania AICT Dayosisi ya Shinyanga Charles Lugembe amewakumbusha wakristo kuwa na utaratibu wa kumshukuru Mungu katika maisha ya kila siku.

Mchungaji Lugembe ameyasema hayo leo wakati akihubiri kwenye ibada ya Jumapili katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.

Amesema ni muhimu kila mkristo kujenga utamaduni wa kumshukuru Mungu katika maisha anayopitia ili kupata baraka zaidi.

“Kuna watu wametendewa mambo makubwa sana walikuwa hawana shule sasa wanashule, walikuwa wanasumbuka na umaskini, walikuwa wanasumbuka na magonjwa Miaka mingi lakini kwa sababu hiyo Mungu amewatendea makubwa lakini kwa kukosa moyo wa shukurani hawana habari tena”.Mchungaji Lugembe

“Nitoe wimbo kwa wakristo tujenge tabia ya kumshukuru Mungu maandiko yanasema mshukuruni Mungu kwa kila jambo unashindwa hata kumshukuru Mungu umemaliza masomo yako salama, unashindwa hata kumshukuru Mungu umemaliza elimu yako ya kidato cha nne au shule ya msingi, unashindwa hata kumshukuru Mungu umeolewa au umeoa, umepata mimba na umepata mototo, unashindwa hata kumshukuru Mungu kwa kupata kazi au unakosa hata kumshukuru Mungu kwa kupata neema ya kuwa kiongozi unakosa hata hilo”.amesema Mchungaji Lugembe

Mchungaji Lugembe pia amewaasa wakristo kuwa na majitoleo kwenye kazi za kanisa  pamoja na shughuli zingine mbalimbali za kijamii.

Mchungaji msaidizi wa Askofu kanisa la Africa Inland Church Tanzania AICT Dayosisi ya Shinyanga Charles Lugembe akiomba katika ibada ya leo Jumapili Januari 8,2023.

Askofu wa makanisa ya AICT Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota wakati akimshukuru Mungu kwa niamba ya kanisa leo kwenye ibada ya Jumapili.

Waumini wakiwa kwenye ibada ya Jumapili Januari 8,2023 katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.





Previous Post Next Post