Kodi Pamoja na tozo mbalimbali ni sehemu ya kukuzia uchumi wa Nchi endapo wananchi wataelimishwa vizuri umuhimu wa kulipa kodi na ni muhimu Tunapotafakari Hapa tutafakari na kuona umuhimu wake.
Dkt Nchemba ametoa kauli hiyo Leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye Kongamano la Kodi la kitaifa lenye lengo la kuongeza ushirikishwaji wa wadau katika ukusanyaji wa maoni Kwa ajili ya maandalizi ya Bajeti Kwa Mwaka 2023/2024.
Dkt. Mwigulu amesema kuwa Kwa mujibu wa historia mambo mengi yalikuwa yanawezwa kufanywa na serikali jambo ambalo watu wakawa na imani ya kuwa serikali inawaajiri wanafunzi kila wanapomaliza vyuo.
Aidha meongeza kuwa mtazamo wa Mhe Rais pindi anapotokea Mtu anaanzisha shughuli za uzalishaji ni vyema watumishi wa serikali wakaonyesha ushirikiano kwa wadau hao ikiwa ni pamoja na kuangalia changamoto walizonazo ili kuzikwamua waweze kujikwamua kwa kupitia Masuala ya kodi na tozo za serikali.
Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Laurence Mafuru amesema wataendelea kushirikiana na sekta binafsi kwani ndio mwajiri na mzalishaji mkubwa katika nchi.
Amesema serikali imekuwa ikiwashirikisha wadau wa sekta binafsi katika mchakato wa kuanza kutengeneza sera za Kodi Ili kuongeza tija katika ukuaji wa uchumi wa Nchi.
“Tunaweza kupanga matokeo ya kodi na mawazo yatakayopatikana ndio yatakayotumiwa na Timu yetu ya Wataalamu ambayo inaandaa sera za kodi kwa mwaka ujao wa Fedha,”amesema Lawrence Mafuru.