Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga
Askari wa Jeshi la
Polisi wakiongozwa na kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Shinyanga kamishina
msaidizi wa Polisi Janeth Magomi wameshiriki kupanda miti Elfu moja ikiwa ni hatua ya kukabiliana na mabadiliko tabia Nchi
Shughuli hiyo imefanyika leo Ijumaa Januari 13,2023
ambapo askari wa Polisi kwa kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wadau
mbalimbali wamepanda miti Mia mbili (200) katika eneo la kambi ya kutuliza
Gasia (FFU) jina maarufu Bwalo la Polisi pamoja na miti Mia nane kwenye eneo la Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga iliyopo kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga .
Akizungumza baada ya
kupanda miti hiyo katika eneo la Bwalo la Jeshi la Polisi na kwenye mazingira
yanayozunguka Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga eneo la Mwawaza,kamanda
Magomi amesema hatua hiyo ni mkakati unaolenga kuhifadhi mazingira
Kamanda Magomi Magomi
amefafanua zaidi kuwa pamoja na majukumu mengine lakini utunzaji wa mazingira
ni mpango endelevu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga
Ameeleza kuwa hatua hiyo pia ni kuunga mkono serikali kupitia kampeni ya
upandaji miti ambapo amesema jeshi hilo limejipanga kukabiliana na mazingira ikiwemo
kuwachukulia hatua watu wanaobainika kuharibu mazingira.
“Tupo
hapa kwa ajili ya kumuunga mkono mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan katika suala zima la kupambana na mabadiliko ya
tabia Nchi, Shinyanga ya kijani inaweekana Shinyanga bila ukame inawezekana”.
“Jeshi
la Polisi tumejipanga kupambana na mazingira lakini tunaendelea kuwaunga mkono
viongozi wetu kuhakikisha kwamba tutaendelea kupanda miti na zoezi hili ni
endelevu na wale wote ambao wataenda kinyume kukata miti bila kibali tuko
tayari kuwashughulikia”.amesema kamanda Magomi
Mkuu wa Wilaya ya
Shinyanga Jasinta Mboneko ambaye ameshiriki katika zoezi la kupanda miti hiyo,
ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuhusu wajibu wa
kuzuia uharibifu wa mazingira, ikiwa ni pamoja na kuepuka ukataji holela wa miti huku
akiwasisitiza wakazi wa Manispaa ya Shinyanga
kuzuia uzurulaji wa mifugo na kwamba jukumu la utunzaji mazingira nila kila
mtu.
“Tuhakikishe
miti hii inakuwa na kuhakikisha kwamba kampeni hii ya miti inaendelea katika Wilaya ya Shinyanga
niendelee kuwaomba wananchi katika maeneo ya kata zetu zote ni marufuku kukata
miti bila kibali na wale wote ambao
wanatembeza mifugo kwenye maeneo mbalimbali ya mitaa na vijiji katika Halmashauri yetu ya Manispaa ya
Shinyanga ni marufuku kupitisha mifugo kwa sababu kwanza inachafua mazingira
lakini pili inakula miti yetu tunataka kuona miti yetu inaendelea kukua”.
“Sheria
zipo za Halmashauri kuhakikisha kwamba wale wote ambao wanatembeza mifugo nah
ii miti inaharibika wanachukuliwa hatua pamoja na wale wa mbuzi kwahiyo
wananchi wote wahakikishe kwamba wanafuga mifugo kwenye nyumba zao”.amesema
DC Mboneko
Afisa mazingira wa
Halmashauri ya manispaa ya shinyanga Ezra Manjerenga amesisitiza umuhimu wa
upandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko alama itakayodumu kizazi hadi
kizazi.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa
wa Shinyanga Dkt. Luzila John ameshukuru na kupongeza hatua hiyo ya Jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga ambapo ameahidi kuilinda ili kuja kuleta manufaa katika
jamii na Taifa kwa ujumla.
Baadhi ya wadau walioshiriki katika shughuli hiyo ya upandaji wa miti
wakiwemo viongozi wa serikali za mitaa pamoja na Jeshi la jadi Sungusungu wameahidi kushiriki katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira
Huku baadhi ya wananchi wakilipongeza jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kutambua umuhimu wa miti katika maeneo hayo ambapo
wamesema wataendelea kuungana mkono kampeni hiyo ili kufikia malengo
yaliyowekwa na serikali.