RAIS DKT. SAMIA AFANYA MABADILIKO YA VIONGOZI

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya nafasi za uongozi katika Serikali ambapo amemteua Balozi Hussein Othman Katanga kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York, nchini Marekani na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa.


Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu Zuhura Yunus leo Jumanne Januari 03, 2022 imeeleza kuwa Balozi Katanga amechukua nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston ambae uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huu balozi Katanga alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Previous Post Next Post