RASMI KLABU YA SIMBA YAMTANGAZA KOCHA ROBERTINHO OLIVERIRA

 



RASMI Klabu ya Simba imemtangaza kocha Robertinho Oliveira kuwa kocha wao mkuu kupitia mkutano mkuu wa waandishi wa Habari uliofanyika leo Januari 3,2023.

Kocha huyo anakuja kuchukua nafasi ya Zoran Maki aliyebwaga manyanga hapo mwanzoni mwa msimu huu.

Kocha huyo mpya ni raia wa Brazil na alikuwa anaifundisha Klabu ya Vipers ya Uganda ambayo ameachana nayo tayari.

Ataungana na Juma Mgunda ambaye alikuwa ni kocha wa muda kwenye benchi a ufundi la timu hiyo ambayo kwa sasa ipo Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi 2023.

Previous Post Next Post