SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UINGIZAJI WA CHUMVI NCHINI

 


Serikali imepiga marufuku uingizaji wa chumvi nchini baada ya inayozalishwa kukosa soko hivyo kupelekea kushuka bei na kusababisha kuathiri uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Uzalishaji wa chumvi nchini ni tani 114 kwa mwaka kwa wenye viwanda lakini mahitaji ni 230 bado hatujawa na takwimu sahihi ya uzalishaji wa chumvi ghafi nchini.

Kauli hiyo ameitoa leo katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mtwara Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Bishara Dr Ashatu Kijaji ambapo alisema Serikali inaweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wanapatikana wawekezaji wa chumvi nchini ili kuondokana na mnunuzi mmoja.


“Nchi inazalisha chumvi ya kutosha nina ombi kwa wazalishaji huwezi kupanga mipango bila kuwa na takwimu sahihi kaeni pamoja tuwe na takwimu sahihi za uzalishaji wa chumvi ndani ya nchi yetu hatuna upungufu wa chumvi ghafi.” Alisema Dr Ashantu na kuongeza,

“Kwanini tuliruhsu chumvi kutoka nje ya nchi mwaka 2008 na janga la elinino ilipelekea tuagize chumvi kutoka nje ya nchini”

“Tumekubaliana kuwa sasa ni mwisho kuleta chumvi ghafi kutoka nje hatuna sababu ya kuendelea kuruhsu chumvi ghafi kuleta ndani ya nchi sasa ni mwisho kuleta kama anaagiza awe amenunua chumvi yote kutoka ndani ya nchi.”

Naye Naibu Waziri Madini Dr Stephen Kiruswa alisema kuwa kumekuwa na taarifa kuwa chumvi inayozalishwa nchini haina viwango na ubora wa kutosha.

“Chumvi inayozalishwa ndani haina tofauti na chumvi inayotoka nje ya nchi hivyo mwekezaji asitafute sababu ya kutonunua chumvi ghafi nchini.” Alisema Dr Kiruswa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazalishaji Chumvi Mkoa wa Mtwara. Hawa Ghasia alisema kuwa pamoja na uzalishaji mzuri wa msimu huu lakini tumelazimika kufunga msimu mapema kwakuwa hatuna soko na hatuna maeneo ya kuhifadhia.


“Gharama zimepanda hata vibarua nao malipo yao ni shilingi 400 tunashindwa kuwalipa kwakuwa hatuuzi chumvi bei ni ndogo tuliwahi kuuza kilo 50 kwa 15 kwa miaka ya nyuma tena mteja anakuja shambani.” alisema Ghasia

Naye Mkaguzi wa Jeshi la Magereza kutoka Gereza la Chumvi Mtwara, Josephat Kanyangenge alisema kuwa wanao uzalishaji mkubwa lakini wanakosa soko la kuuzia chumvi hiyo.

“Kutokana na changamoto ya soko la chumvi ghafi tulilazimika kufungua kiwanda cha kuchakata chumvi tunayozalisha ingawa tumeshindwa kuichakata kutokana na mashine zetu ambazo sio bora endapo tukipata mashine bora tunaweza kufanya vizuri zaidi.” alisema Kanyangenge.




Chanzo - Mwananchi

Previous Post Next Post