CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) MKOA WA
SHINYANGA.
Baraza la Uongozi la CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, limepokea kwa furaha taarifa ya mwenendo wa maridhiano baina ya chama chetu na serikali ambayo yamepelekea kuondolewa kwa zuio haramu la kutokufanya mikutano ya hadhara kwa Chama cha CHADEMA, pia kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali, pamoja na suala la Katiba.
Aidha, Baraza la Uongozi linapenda kutoa salamu za pongezi na shukrani nyingi kwa Mhe Freeman Aikael Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA Taifa, kwa moyo wake wa kipekee na ujasiri katika kuasisi na kusimamia mazungumzo haya kwa upande wa Chama. Tunaamini hitimisho hili zuri la matokeo haya, linatoa mwanga wa matumaini kuelekea kufanikiwa kwa mambo mengine, likiwemo la upatikanaji wa Katiba Mpya itakayozaa Tume Huru ya Uchaguzi
Vile vile, Baraza la Uongozi Mkoa wa Shinyanga, kama ilivyokuwa awali wakati mazungumzo haya yanaanza, linaendelea kuwaunga mkono na kuwatia moyo viongozi wetu wote waliopo katika michakato yote ya maridhiano inayoendelea.
Tanzania ni yetu sote, tuna wajibu wa kuilinda na kukilinda Chama chetu kwa wivu mkubwa.
Pamoja na salamu za chama.
Imetolewa leo 04 Januari, 2023 na;
Emmanuel Ntobi
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi
Mkoa wa Shinyanga