VIONGOZI WA DINI SHINYANGA WAKUMBUSHA SIRI ZA MAFANIKIO MWAKA 2023

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Askofu wa makanisa ya Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota amewakumbusha wakristo na jamii kuendelea kudumisha amani ya Nchi katika Mwaka  huu 2023 ili kuvuka salama.

Ametoa rai hiyo katika ibada ya sikukuu ya mwaka mpya iliyofanyika kwenye kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga ambapo Askofu Bugota amesema ni muhimu kila mtu kuilinda kwa kuiishi amani ya Tanzania ambayo ipo tangu zamani Miaka ya nyuma.

Askofu Bugota amewasisitiza wakristo wote kuendelea kumuomba Mungu kuombea Taifa amani iendelee na kwamba katika Mwaka huu mpya 2023 watu wanapaswa kuacha kutenda matendo mabaya hali hiyo itachangia kuumaliza Mwaka katika hali ya usalama.

Katika mahubiri yake mgeni ambaye ni katibu wa AICT Dayosisi ya Mwanza Mchungaji Philipo Kamwele amesema Mwaka huu 2023 ni muhimu kila mtu kuishi kwa kuweka alama zenye mafanikio katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Mchungaji Kamwele amesema siri kubwa ya mafanikio katika kuishi hapa Duniani ni kutumia vizuri muda ambao ni zawadi ya Mungu kwa kila mtu pamoja na kutumia nafasi au fursa mbalimbali kuleta mafanikio katika maisha ya kila siku.

Amesisitiza wakristo kuishi katika maisha yanayompendeza Mungu huku akiwakumbusha kumshukuru Mungu katika kila hatua ikiwemo hatua ya mafanikio na wakati wa changamoto kwa kusimama imara kiimani.

Askofu wa makanisa ya Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga ambaye pia ni makamu Askofu mkuu wa Tanzania Zakayo Bugota akizungumza kwenye ibada katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.

Katibu wa AICT Dayosisi ya Mwanza Mchungaji Philipo Kamwele akihubiri kwenye ibada katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.

Katibu wa AICT Dayosisi ya Mwanza Mchungaji Philipo Kamwele akihubiri kwenye ibada katika kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga.

Mchungaji Charles Lugembe wa kanisa la AICT Kambarage ambaye pia ni mchungaji msaidizi wa Askofu Dayosisi ya Shinyanga akiongoza ibada katika kanisa hilo.





Previous Post Next Post