Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Wajasiliamali katika soko jipya la Mnara wa Voda
karibu na ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga mjini wameipongeza serikali kwa
kuendelea kuboresha miundombinu ya soko hilo hali ambayo itachochea uchumi.
Hayo wameyazungumza baada ya Misalaba Blog
kutembelea katika soko hilo ambapo baadhi ya wajasiliamali wamepongeza juhudi
zilizofanywa na viongozi wa chama na serikali
kwenye kuboresha miundominu ya soko hilo.
Wamesema hatua hiyo itawasaidia kufikia malengo yao
kwa kuinuka kiuchumi kupitia biashara ambapo pia hali hiyo itasaidia kuinua
uchumi wa Halmashari ya Manispaa ya Shinyanga kupitia mapato ya ndani.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa soko hilo
Bwana Omary Mussa naye amepongeza juhudi za serikali kufikia hatua ambapo
ameomba maboresho hayo yaendelee sehemu zenye changamoto.