Wamesema kukosekana kwa
vivuko hivyo imekuwa ikiwalazimu wanafunzi hao
kuruka mitaro ambayo ni mirefu
hali ambayo ni hatari kwa usalama wao hasa kwa watoto wadogo.
Kwa upande wake mjumbe
wa serikali ya mtaa wa Mbuyuni akizungumza kwa niamba ya mwenyekiti wa mtaa
huo, Angelina Makwaiya amewataka watumiaji wa vyombo vya moto wanaotumia
Barabara zinazopakana na shule za Msingi Bugoyi
A na B kuzingatia sheria za usalama Barabarani ili kuepusha ajali
zinazoweza kuzuilika hasa kwa wanafunzi.
Watumiaji wa vyombo vya moto zikiwemo Gari,pikipiki na Baiskeli wamelalamikiwa kwa tabia ya kutozingatia sheria za usalama Barabarani hasa katika maeneo yanayopakana na shule,hivyo kusababisha hofu kwa wazazi na walezi.