WAZIRI MABULA AAGIZA HALMASHAURI KUTWAA MAKAZI NA MAPORI YASIYO ENDELEZWA MJINI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiongea na Makampuni pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa programu ya urasimishaji makazi yasiyopangwa nchini kilichofanyika leo jijini humo katika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiongea na Makampuni pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa programu ya urasimishaji makazi yasiyopangwa nchini kilichofanyika leo jijini humo katika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa.Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi akiongea na Makampuni pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa programu ya urasimishaji makazi yasiyopangwa nchini kilichofanyika leo jijini humo katika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa mapema leo.Sehemu ya Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Makampuni yalioshiriki kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa programu ya urasimishaji makazi yasiyopangwa wakifuatilia jambo kwa makini kuhusu urasimishaji jijini Dar es Salaam.

************************

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula ameziagiza mamlaka za Kupanga, Kupima na Kumilikisha ardhi nchini kuyatambua maeneo au viwanja ambavyo havijaendelezwa katika maeneo ya mijini yatambuliwe na kunyanganya milki zake ili zigawiwe kwa wengine wenye uwezo wa kuziendeleza.

Waziri Mabula amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa programu ya urasimishaji makazi yasiyopangwa nchini kilichofanyika leo jijini humo katika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa.

Waziri Mabula akiongea mbele ya makampuni ya urasimishaji jijini Dar es Salaam alibainisha kuwa maeneo haya yasiyoendelezwa yanachafua taswira ya Miji lakini pia yanapoteza mapato ambayo kama yangeendelezwa yangekuwa na faida kiuchumi.

Aidha Waziri Mabula aliongeza kuwa baada ya Mamlaka hizo kuyatambua maeneo yanayoweka mapori mjini yawasilishe kwake ambaye pia atajiridhisha ili yaweze kutolea kibali cha kuyachukua baada ya kuchunguza na kujiridhisha kuwa yanastahili kutaifishwa.

Dkt. Mabula pamoja na agizo hilo pia amezikumbusha mamlaka husika kuhakikisha mipango ya uendelezaji miji ni lazima izingatie mipango kabambe iliyopo na si vinginevyo.

‘’Kama sehemu imepangwa kujengwa jengo la ghorofa kumi basi lisijengwe jengo la ghorofa ishirini na kama ni ghorofa mbili basi lijengwe la gorofa mbili, ramani kwa ajili mipango kabambe zishatoka hivyo uendelezaji makazi lizingatie hayo’’. Aliongeza Dkt. Mabula Waziri wa Ardhi.

Waziri Mabula katika hotupa yake kwa viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Makapuni hayo alisema Urasimishaji makazi yasiyopangwa nchini ni takwa la kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Na.4 ya mwaka 1999 fungu la 56-60 na Sheria ya Mipangomiji Na.8 ya mwaka 2007 fungu la 23.



Waziri Mabula alibainisha kuwa msingi huu wa kisheria unatokana na Sera ya Taifa ya Ardhi 1995 ambayo inatambua makazi yasiyopangwa na kutamka kuwa yatapangwa na kuboreshwa kupitia mipango shirikishi, isipokuwa yale yaliyojengwa kwenye maeneo hatarishi.



Waziri aliongeza kuwa Sambamba na Sera ya Ardhi, Sera ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000 inaelekeza kuwa maeneo yaliyoendelezwa bila kupangwa yatarasimishwa kwa kushirikisha wananchi ili kuboresha makazi yao.

Waziri Mabula aliutaja Mkoa wa Dar es salaam kuwa ni moja ya mikoa muhimu katika mazoezi ya urasimishaji yanayoendelea nchini kote akiongeza kuwa kuna jumla ya Kampuni za Upangaji na Upimaji 86 zinatekeleza kazi za urasimishaji katika mitaa 272 ya halmashauri tano za Dar es salaam.

Aidha Waziri Mabula alisema takriban asilimia 24 ya kazi zote za urasimishaji nchini zinafanyika katika mkoa wa Dar es salaam na hadi sasa jumla ya viwanja 554,738 vimepangwa na kurasimishwa kupitia michoro 2,084 ya urasimishaji. Kati ya hivyo, viwanja 108,193 upimaji wake umekamilika na kuidhinishwa ambavyo ni sawa asilimia 20 ya vile vilivypangwa.

Waziri Mabula aliongeza kuwa asilimia 80 ya viwanja vilivyopangwa bado viko katika upimaji wa awali akiongeza kuwa jumla ya hati 25,083 zimeandaliwa ambazo ni sawa na asilimia 23.2 ya viwanja vyote vilivyopimwa.



Naye Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi wakati akimkaribisha Waziri kufungua mkutano huo alisema kikao kazi hicho kipo kuwasilisha, kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu Mkakati ulioandaliwa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokabili zoezi la urasimishaji katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Dkt. Kijazi alibainisha kuwa Kikao kazi hii inaanzia Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na ukubwa na wingi wa watu ambao ni takribani 8.5% na mchango wake katika uchumi wa nchi, ni 23.5% ya makazi yote yaliyorasimishwa nchini yako Dar es Salaam.

Dkt Kijazi ana matumaini kuwa Mamlaka za upangaji zitadhibiti ujenzi holela ili kuhakikisha utekelezaji wa mpango kabambe utafuatwa akibainisha kuwa baada ya kikao hicho atakuja na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha ile asilimia 80 ya kazi ambazo hazijakamilika inakamilika.
Previous Post Next Post