VINARA wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Yanga SC imeanza vyema katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi CUP 2023 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMKM mchezo uliopigwa uwanja wa Amani mjini Zanzibar.
Yanga wamepata bao katika dakika za lala salama 90+5 likifungwa na Dickinson Ambundo
Kwa ushindi huo Yanga wanahitaji ushindi dhidi ya Singida Big Stars ili kutinga hatua ya nusu fainali.
Singida Big Stars wanaongoza Kundi wakiwa na Pointi 3 sawa na Yanga ila wakiwa na uwiano wa kufunga mabao.