" MAYELE ASHINDA GOLI LA WIKI SHIRIKISHO

MAYELE ASHINDA GOLI LA WIKI SHIRIKISHO

 


Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ameibuka mshindi wa goli la wiki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, raundi ya tano

Mayele ameshinda tuzo hiyo kupitia goli alilofunga kwenye mchezo dhidi ya US Monastir uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0

Lilikuwa bao la pili akipiga shuti kali baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Kennedy Musonda akiwa nje kidogo ya 18

Lilikuwa bao lake la tatu kwenye hatua ya makundi michuano ya kombe Shirikisho barani Afrika

Post a Comment

Previous Post Next Post