
Na Suzy Luhende, Misalaba Blog
Wananchi zaidi ya 1147,450 wamefaidika na huduma ya maji katika mkoa wa Shinyanga ambapo zaidi ya Sh 52 Bilioni zimetolewa na serikali ya awamu ya sita kwa ajili ya utejelezaji wa miradi ya maji mkoa wa Shinyanga huku miradi mbalimbali ikiwemo sekta ya barabara, sekta ya afya na sekta ya elimu ikitekelezeka kwa wakati, katika kipindi chà awamu ya sita
Hayo yabebainishwa Machi 25,2023 na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, kwenye kongamano la miaka miwili ya mafanikio ya Utawala wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan lililofanyika kimkoa Mjini Shinyanga na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wakiwamo Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga.
Akieleza mafanikio ya Mkoa wa Shinyanga Mndeme ndani ya miaka miwili ya Rais Samia, amesema zimeletwa fedha nyingi na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi ikiwemo miradi ya sekta ya maji ambapo jumla ya wananchi 1147,450 wamefaidika na huduma hiyo mkoani Shinyanga.
Akizungumzia mafaniko katika Sekta ya Maji, amesema Rais Samia ametoa kiasi cha fedha Sh. 52.2 bilioni na kutekeleza miradi ya maji 45, na katika mwaka wa fedha (2021/2022) RUWASA ilipokea Sh 29.5 bilioni na kutekelezwa miradi ya maji 29, pia kuna ujenzi wa miradi mipya ya maji 15 yenye thamani ya Sh.bilioni 24.3.
Amesema pia katika mwaka wa fedha (2022/2023) RUWASA Mkoa walipokea fedha Sh.22.7 bilioni na kutekelezwa miradi ya maji 15 na kuondoa adha ya wananchi kutumia maji yasiyofaa.
Amesema katika Sekta ya Afya, serikali ya Rais Samia imetoa kiasi cha fedha Sh.32.6 bilioni na kujengwa vituo mbalimbali vya Afya na Zahanati, pamoja na Sh.7.8 bilioni kujengwa Hospitali ya Rufaa mkoani humo, na kuondoa na adha ya wananchi kufuata huduma za matibabu Bugando Jijini Mwanza na Mhimbili, ambapo pia kiasi cha fedha Sh. 14.9 bilioni zilitolew na kununua vifaa tiba pamoja na madawa hivyo kuwa na asilimia 89 ya upatikanaji wa madawa.
Akizungumzia Sekta ya Elimu amesema Rais Samia ametoa fedha Sh.37.6 bilioni na kuboresha miundombinu ya elimu ikiwamo ujenzi wa matundu ya vyoo, madawati, vyumba vya Madarasa, huku akitoa Sh. 2.2 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Kishapu, pamoja na Shule mpya ya Sekondari ya Wasichana iliyopo Butengwa Manispaaya Shinyanga.
Aidha Mndeme ameelezea mafaniko ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, amesema Rais Samia ndani ya miaka miwili, zimejengwa barabara nyingi ikiwamo ujenzi wa Makaravati, Madaraja pamoja na uwekaji wa Taa za Barabarani.
“Kwa kweli Mkoa wa Shinyanga ndani ya miaka miwili ya utawala wa Rais Samia tunajivunia mafaniko makubwa ya kimaendeleo pamoja na mapinduzi ya kiuchumi, ikiwamo na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) pia ametoa fedha Sh.21 bilioni kwa ajili walengwa wa mpango wa kunusuru Kaya maskini TASAF, huku zikitolewa Lesseni za uchimbaji madini 827 na Lesseni za wachimbaji wadogo 267,”amesema Mndeme.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amempongeza Rais Samia kwa kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa vitendo, na wameona mvua kubwa ya maendeleo na wataendelea kumuombea afya njema ili aendelee kuwatumikia vyema watanzania.
Akizungumza kwa niaba ya wabunge wa mkoa wa Shinyanga Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi katika Mkoa huo na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.
Baadhi ya wananchi Joseph Martine na Jalia Musa wamemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo hivyo wamemuomba aendelee kuwajali wanyonge na akemee ushoga usiendelee kuwepo katika nchi ya Tanzania kwa sababu sio mira na desturi ya watanzania.
Post a Comment