
Na. Elias Gamaya, Shinyanga
Katika kuhakikisha jamii inaondokana
na vitendo na viashiria vya ukatili wa kijinsia taasisi ya Shujaa wa Maendeleo
na Usitawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa shinyanga imefika chuo kikuu cha
Ushirika Moshi (MoCU) tawi la Shinyanga lililopo halimashauri ya manispaa ya
Shinyanga mkoani humo kutoa elimu ili kuwawezesha wanachuo wajue athari za
ukatili.
Akizungumza wakati wa Semina Katibu
Wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Masunga Dotto Mazoya amewasihi wanachuo kuepukana
na mapenzi ya jinsia moja(Ushoga na Usaganaji) yanayoharibu taifa letu ambapo
kawaasa wanachuo kuachana na mila na desturi za kigeni na kusema kua Tanzania
Bila ukatili inawezekana.
" tuache mambo ya kukopikopi mila na desturi za wazungu,
simu zetu tuzitumie kwa ajili ya mambo ya msingi wala si kwa ajili ya kuangalia
picha zisizo faa" Amesema Katibu SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Mazoya.
Mwenyekiti idara ya michezo SMAUJATA
Mkoa wa Shinyanga Alkwin Wille amebainisha aina za Ukatili ikiwemo Ukatili wa
kingongo, Ukatili wa Kiuchumi, Ukatili wa kimwili na Ukatili wa kisaikolojia
ambapo kasema ili kuwa baba au mama wa kesho lazima tuwe mabalozi kwa jamii juu
ya vitendo na viashiria vya Ukatili.
Kwa upande wake Katibu wa idara ya michezo
SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Meshack Kwanja amesema maranyingi ukatili
unasababishwa na watu waliokalibu, ndugu au jamaa wa karibu
"Maranyingi ukatili
unafanywa na watu waliokatibu yetu hivyo ni jukumu ka kilammoja wetu kuibua na
kupinga vitendo vya ushoga kwa kupiga namba ya bure 116 nchi nzima" amesema Meshack Kwanja Katibu wa idara ya
michezo SMAUJATA mkoa wa Shinyanga.
Nao baadhi ya washiriki wa semina hiyo
wameeleza namna ambavyo elimu hiyo itawasaidia kutokomeza ukatili wa kijinsia
huku wengine wakiiomba serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wale wote
wanaofanya ukatili wa kijinsia , kuweka jitihada za uelimishaji dhidi ya
ukatili kwenye mashirika yanayopinga vitendo hivi.
" mimi kama mama
mtarajiwa nimefurahi na elimu iliyotolewa ambayo itanisaidia katika malezi ya
watoto wangu pia naweza kua mjumbe katika kuelimisha kwenye jamii kupinga
ukatili wa jamii" amesema Salome Jackson mwanachuo. (MoCU) tawi la
shinyanga.

Katibu Wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga
Masunga Dotto Mazoya akizungumza kwenye semina hiyo.

Katibu Wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga
Masunga Dotto Mazoya akizungumza kwenye semina hiyo.


Post a Comment