" MKUTANO KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA (SPC) NA WADAU, MAADHIMISHO UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MKUTANO KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA (SPC) NA WADAU, MAADHIMISHO UHURU WA VYOMBO VYA HABARI


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) leo Alhamisi Mei 18,2023 inaadhimisho  siku ya uhuru wa vyombo vya habari Mkoa wa Shinyanga.

Maadhimisho hayo yana ambatana  na kauli mbiu “Kuunda Mustakabali wa haki, uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha haki nyingine zote za kibinadamu”.

Maadhimisho hayo yanafanyika katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kwamba yanaadhimishwa kwa njia ya mkutano uokwenda sanjali na mjadala wa mada isemayo “Uhuru wa kujieleza ni ustawi wa maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga” ambapo washiriki kutoka sekta mbalimbali watabainisha maeneo yanayopaswa kufikiwa na vyombo vya habari.

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Mkoa wa Shinyanga ni mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akimwakilishi mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) ni mdau mkubwa wa maendeleo kwa Mkoa wa Shinyanga kwa kujikita katika shughuli za uhabarishaji kwa jamii na kuunganisha jamii na serikali kupitia kalamu ya vyombo vya habari.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akifungua mkutano katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga leo Mei 18,2023.

Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) Bwana Greyson Kakulu akisoma risala.

 

Mkutano maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Mkoa wa Shinyanga ikiendelea leo Alhamisi Mei 18,2023.




Post a Comment

Previous Post Next Post