
Na
Elisha Petro
Michuano
ya Umiseta manispaa ya Shinyanga
imetimua vumbi katika uwanja wa CCM Kambarage mkoa wa Shinyanga kwa
michezo tofauti kucheza ikiwemo mpira wa miguu (Football),mpira wa wavu (Volleyball)
pamoja na mpira wa pete (Netball).
Mchezo
wa mpira wa miguu Shule ya sekondari Mwasele imefanikiwa kutwaa kombe baada ya
ushindi wa goli 3-0 walioupata kufuatia
kichapo walichokitoa kwa wapinzani wao kutoka Shule ya sekondari Old Shinyanga.
Edward Mashenene kocha na mwalimu wa michezo katika shule ya sekondari
Mwasele amewapongeza vijana wake kwa kazi nzuri walioifanya kwa kuibuka na
ushindi licha ya mchezo huo kuwa wa ushindani zaidi na ameahidi kuwa mashindano
ya msimu ujao watafanya vizuri zaidi ya walichokifanya msimu huu.
"Mimi huwa nakaa na vijana na binafsi niwapongeze wachezaji wangu kwa walichokifanya leo huu ulikuwa mchezo mgumu sana kwetu kwani tulilazimika kufanya mabadiliko mapema leo kwa sababu tuliyemfanyia mabadiliko mlinda mlango wetu number moja aliumia mapema wakati wa wrm up lakini kilichofanyika leo msimu ujao itakuwa zaidi ya hiki naahidi kuwafunga sana"
Kwa
upande wake Simba Selemeni kocha wa timu wa timu ya Mwasele sekondari
amewapongeza wapinzani wake kwa kupata matokeo mazuri katika mchezo huo na
kuahidi kujipanga zaidi msimu ujao kwa lengo la kufanya vizuri zaidi ya kile
walichokionyesha katika mchezo huo.
"Naipongeza timu ya Mwasele wamepata matokeo na
wamecheza mpira mzuri wenzetu ni timu ya muda mrefu wanamuunganiko mzuri na
wanavyocheza inaonyesha kabisa kuwa walichokipata leo ni matunda ya maandalizi
yao mazuri sisi tulianza na wachezaji kidato cha kwanza lakini wamejitahidi
binafsi niwaombe wazazi na hata walimu kuwaunga mkono wanafunzi katika michezo
yote sisi tutarudi imara zaidi"
Kwa
upande wa mpira wa wavu wasichana wa shule ya sekondari Ngokolo wameibuka kifua
mbele baada ya ushindi wa seti 3-0 dhidi
ya shule ya sekondari Chamaguha lakini pia timu ya mpira wa wavu kwa wavulana
kutoka shule ya Ngokolo wamefanikiwa kupata ushindi wa set 3-0 dhidi ya shule
ya sekondari Chamaguha.
Kwingineko
katika mpira wa pete vijana kutoka shule
ya Sekondari Mwasele wamepeperusha vyema bendera ya timu yao kwa ushindi wa
jumla ya goli 48 – 23 dhidi ya timu kutoka shule ya sekondari Masekelo.
Mganga
hajigangi hatimaye waalimu wakubali kufundishwa soka baada ya kupokea kichapo
cha goli 3-1 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kambarage.
Afisa
michezo Manispaa ya Shinyanga Arnold Ruzika ametoa baadhi ya changamoto
mbalimbali kwa mgeni rasmi ambaye ni
Afisa Elimu sekondari Manispaa ya shinyanga ikiwa ni pamoja na kuboresha ulinzi la usalama katika maeneo yote yatakayokuwa yanatumika
kwa michezo ya Umiseta.
"Kwanza changamoto ya kwanza ni suala la ulinzi na usalama
kuna vijana wengi ambao sio wanafunzi wanaoshiriki nasi lakini wamekuwa
wakihatarisha usalama wa wanafunzi msimu huu kuna baadhi ya wanafunzi
wamejeruhiwa na tayari waliohusika katika hilo wapo mikononi mwa sheria, pia kuna
wanafunzi wanapoteza vipaji vyao kutokana na baadhi ya walimu kuwazuia
kushiriki katika haya mashindano lakini haya mashindano hayawezi kumuathiri
mwanafunzi kitaaluma kwa sababu walimu wanapaswa kuwaandaa wanafunzi vizuri
katika masomo na sio kuwazuia kushiriki mashindano na mwisho kuna baadhi ya
shule hazina vifaa vya michezo kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya
michezo kwa vijana wetu"
Aidha
Afisa Elimu sekondari manispaa ya Shinyanga Cleophace Mzungu ametoa maagizo kwa
wakuu wa shule zote kuhakikisha wananunua vifaa vyote vya michezo na kuahidi
kuwa atapita shule moja baada ya nyingine ili kukagua utekelezaji wa zoezi
hilo.
"Tuendeleze
utaratibu wa kuendesha mashindando mashindano haya ngazi ya shule,kata,wilaya
na ngazi ya taifa ili tupate vipaji bora zaidi mimi binafsi na ofsi ya
mkurugenzi tunaahidi kuwapa ushirikiano pale ambapo mtakuwa mmekwama kunatatizo
la baadhi ya shule kutokuwa na vifaa vya michezo natoa agizo na sio ombi kila mkuu wa shule ahakikishe ananunu vifaa vya
michezo kwa mwaka huu itakapofika mashindano ya msimu ujao kila shule iwe na
vifaa vya michezo na nitafanya ukaguzi kwa kushirikiana na uongozi wa
Halmashauri"
Mwisho
wa michuano ya Umiseta ngazi ya wilaya iliyochezwa katika uwanja wa CCM
Kambarage ni mwanzo wa maandalizi ya mashindano hayo ngazi ya Mkoa
yanayotarajiwa kutimua vumbi katika uwanja wa chuo cha ualimu ShyCom uliopo
Shinyanga mjini.

Post a Comment