Na Elisha Petro.
Imeelezwa kuwa hali ya mmomonyoko wa maadili imechangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo wazazi kutowajibikia jukumu la malezi na makuzi kwa watoto, na badala yake kujikita zaidi kwenye shughuli za kutafuta kipato
Hayo yamesemwa na washiriki wa mdahalo
uliohusisha wadau mbalimbali katika kujadili mada inayohusu kuporomoka kwa
maadili katika jamii.
Kaimu Mkuu wa Chuo Sayansi za Afya kolandoto,Michael Henerco anasema kuwa changamoto ya mmomonyoko wa maadili inawahusu watu wote katika jamii kufuatia agizo la serikali ya Tanzania katika kujadili hali ya mmomonyoko wa maadili nchi na unatekelezwa katika vyuo vyote na leo chuo cha kolandoto kimechukua hatua.
" Hii changamoto ya
kuporomoka kwa maadili inatuhusu sisi sote kwa sababu imetuathiri na wengine
wanapoteza maisha yao na utu tulifurahishwa
na agizo la serikali kwa ajili ya kujadili hali ya mmonyoko wa maadili kwa kuwa
kila mmoja hapa anaguswa na athari hizi na tumealika wataalam wabobezi wa
masuala haya ili ya kuweza kujadiana na kupata maoni kwa
washiriki kutoka makundi mbalimbali"anasema
Henerco
"Tunaomba
washiriki wote kuweza kutoa maoni ili tuweze kujifunza na tuondoke hapa tukiwa
mabalozi kwa kusimamia jamii yetu kuhusu hali ya maadili na si
wakati kunyamaza kwa hali maadili ilivyo kwa sasa kwa kuwa kila
moja wetu hili lina mhusu"Anasema Henerco.
Kaimu mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Michael Hernerico akifungua mdahalo wa mmomonyoko wa maadili nchi.
Akichangia katika mdahalo huo juu ya chimbuko la mmomonyoko wa maadili kwa mujibu
wa neno la Mungu Mchungaji wa Chuo cha sayansi za Afya Kolandoto Joel
Luginya amebainisha kuwa matendo
yasiyompendeza Mungu yanachangia kuporomoka kwa maadili katika jamii.
‘Mmomonyoko
maana yake ni ukiukwaji wa maelekezo yaliyowekwa na Mungu au kiongozi kutoka
katika jamii flani kwa ajiri ya maendeleo ya ustawi wa jamii,chimbuko la
mmomonyoko wa maadili lilianzia katika bustani ya Edeni baada ya Adam na Hawa
kushindwa kutekeleza magizo ya Mungu na kusikia Sauti ya muovu ibilisi kitabu
cha Mwanzo 3: 1- 8 kwahiyo mmomonyoko wa maadili mzizi wake ni matokeo ya
dhambi kusingekuwa na dhambi kusingekuwa na mmomonyoko wa maadili lakini Mungu
ametuletea dawa ya mmomonyoko wa maadili kupitia kumwamini Mungu, kuwa na hofu
ya Mungu bila kusahau kumuomba Mungu kwa kuungama na kutubu’
Afisa ustawi wa jamii kutoka wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia,wanawake na makundi maalumu Mkoa wa Shinyanga Sophia Kang’ombe amewasilisha na kuchangia mdahalo katika mada ya pili inayohusu namna saikolojia inavyoathiri tabia na kubainisha kuwa
‘Tabia
ya mtu anakuwa nayo kupitia malezi au kurithi,Mazingira anayokulia kama vile shuleni,katika
maeneo yake ya kazi,nyumbani na hata katika jamii zetu yanaweza kuathiri tabia
ya mtu hata hivyo tunaowajibu wa kuhakikisha makuzi na malezi bora kwa watoto
ili kuepukana na mporomoko wa maadili katika jamii zetu’
"Wana
ndoa waepuke migogoro na watenge muda wa ziada wa kulea watoto na wakubaliane
idadi ya watoto wanaoweza kuwalea kadri ya kipato chao na hata kuepuka kuiga
maisha ya mitandao ya jamii ili tusiharibu watoto"Anasema Lydia.
Kwa upande wake Mrakibu mwandamizi wa polisi Monica Sehere amebeinisha sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha kuporomoka kwa maadili wakati wa kuwasilisha na kuchangia mdahalo huo juu ya ukubwa wa mmomonyoko wa maadili na madhara yake.
‘kukosekana
kwa hofu ya Mungu,kupungua kwa upendo na hata imani za kushirikina ni moja ya
sababu zinazoweza kusababisha mmomonyoko wa maadili lakini kunamadhara makubwa
yanayoweza kutokea maadili yakishuka kwanza tutaathiri mila na desturi za taifa
letu,kukosekana kwa Amani lakini pia tutaathiri maendeleo yetu na taifa kwa
ujumla’
Mkuu wa dawati la jinsia jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SSP Monica Sarehe akiwasilisha mada inayohusu ukubwa wa mmomonyoko wa maadili na madhara yake.
Wakati huohuo Afisa maendeleo ya jamii
mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akiwasilisha na kuchangia mada inayohusu namna maendeleo
yanavyo sababisha mmomonyoko wa maadili amesema
maendeleo ya kidemokrasia na uhuru wa kutumia mitandao ya kijamii ni chanzo
mojawapo katika hilo.
‘Maendeleo
ya kidemokrasia na uhuru wa mitandao ya kijamii imetuweka hapa tulipo kwa sasa
na kutusahaulisha mambo ya msingi badala yake tunaegemea katika mambo
yasiyokuwa ya msingi yanayotumia muda mwingi na gharama kubwa lakini pia
maendeleo ya mtu na vitu yanaongeza ubinafsi na kutufanya tushindwe
kujishugulisha na masuala ya kijamii’
Afisa maendeleo mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akiwasilisha na kuchangia mada inayohusu maendeleo yanavyoathiri mmomonyoko wa maadili nchini.
Ngwale ameongeza kuwa ili jamii ijikwamue
katika hali mbaya ya mmonyoko wa maadili serikali inapaswa kuegemea zaidi
katika ngazi za elimu kuwaelimisha watoto na jamii kwa ujumla.
‘
Niwakati wa taifa kufanya mchopeko wa mataala wa maadili kuanzia ngazi ya msingi
ili watoto wajifunze maadili toka wakiwa shuleni lakini pia Wizara ya sayansi
na technolojia ione namna ya kuendesha hii mitandao ya kijamii ili kuepuka
matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa chuo
cha sayansi ya Afya Kolandoto wamebainisha njia mbalimbali zinazoweza
kutumika katika kulinda maadili nchini ikiwa ni pamoja na kuiomba serikali, wazazi na viongozi wa dini nchini kote kushirikiana.
‘Viongozi
wa Dini zote washirikiane kuisema kweli ya Mungu,Serikali izuie machapisho
potoshi katika mitandao ya kijamii yanayoharibu maadili lakini pia wazazi
wanapaswa kutumia lugha rafiki kwa watoto pamoja na kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao ili
kuwajengea watoto hali ya kujitambua, Pia madawati ya jinsia yaongeze kasi ya
kupambana na mmomonyoko wa maadili kwa kutoa elimu kwa watoto,wazazi na walezi’
Post a Comment