Na Respice Swetu, Misalaba Blog.
Wanafunzi 350 wanaosoma kwenye madarasa ya mpango wa elimu ya msingi kwa walioikosa MEMKWA wilayani Kasulu, wamekabidhiwa msaada wa kalamu na madaftari uliotolewa na mfuko wa maendeleo wa kusaidia kaya masikini TASAF.
Akikabidhi msaada huo afisaelimu watu Wazima wa Wilaya ya Kasulu Simon Kichumu amesema kuwa, kutolewa kwa vifaa hivyo ni kutokana na serikali kutambua uwepo wa watoto wanaokwama kuzifikia ndoto zao kutokana na ukosefu wa vifaa vya kujifunzia.
Walengwa hao wanaosoma katika madarasa yaliyopo kwenye vituo vya shule za msingi za Heru Ushingo, Kigadye, Nyarugusu, Kitanga, Nyamuganza, Mvugwe, Mvinza na Kagera ni miongoni mwa 1446 waliosajiliwa katika halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kupitia mpango huo na kuvuka lengo la kusajili walengwa 802 waliokuwa wametarajiwa.
Akikabidhi vifaa hivyo, Kichumu amewataka walengwa hao kuhudhuria masomo kikamilifu na muda wote pamoja na kuvitumia vifaa hivyo kikamilifu.
Aidha kabla ya tukio hilo, kulifanyika ugawaji wa sare za shule kwa watoto wanaotoka katika mazingira magumu kwenye shule ya Msingi ya Kisuma.
Sare hizo ambazo ni kaptula, sketi na viatu ni matokeo ya juhudi za mwalimu Yusuf Hamis wa shule ya Msingi Kisuma kuwasiliana na wadau mbalimbali ili kutafuta namba ya kuwasaidia watoto hao.
Pamoja na kupatikana kwa sare hizo, Yusuf ameiwezesha shule ya Msingi ya Kisuma kupata ngoma za kisasa kwa ajili ya bendi ya shule zinazotumika shuleni hapo.
Kufuatia kuwepo kwa bendi hiyo, shule ya Msingi ya Kisuma imekuwa miongoni mwa shule ambazo zimemsha ari ya watoto kupenda shule na kuchochea mapambano ya kuinua taaluma, kupanbana na utoro na mdondoko wa wanafunzi.
Yusuph ni mwalimu mwenye ulemavu ambaye katika siku za karibuni, amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kuonekana katika mitandao ya kijamii akifundisha kwa nyimbo, michezo na mbinu anuai na kunfanya kuwa kipenzi cha wanafunzi.
Post a Comment