Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amewakumbusha watawa kuendelea kuwa kielelezo cha upendo wa Mungu kwa Kanisa na watu wake, kupitia maisha ya wakfu waliyoyachagua.
Askofu Sangu ametoa wito huo kwa watawa, wakati akiongoza Misa takatifu ya kuweka nadhiri za kwanza na kurudia nadhiri kwa watawa wapatao 20 katika Shirika la Kijimbo la Maria Mtakatifu Mama wa huruma, ambayo imefanyika mwanzoni mwa wiki hii katika Kanisa kuu la Mama mwe ye huruma Ngokolo mjini Shinyanga.
Askofu Sangu amewataka watawa hao wapya kutambua kuwa, wana jukumu kubwa la kuwa mfano na kielelezo cha maisha ya upendo, utii na unyenyekevu pamoja na kulisaidia Kanisa kupeleka habari njema ya Kristo kwa watu wote.
Askofu Sangu alitumia nafasi hiyo kuwaomba waamini kuendelea kuwaombea watawa hao wapya, ili Mungu aendelee kuwalinda, kuwaangazia nuru ya uso wake, kuwapa amani na kuwawezesha kuyaishi maisha yao ya wakfu.
Kupitia Misa hiyo, jumla ya Watawa 20 walifunga nadhiri zao za Usafi kamili, ufukara na utii katika Shirika la Jimbo Katoliki Shinyanga la Maria Mtakatifu Mama wa Huruma, ambapo 14 kati yao walifunga nadhiri za kwanza huku wengine 6 wakirudia nadhiri zao.
Waliofunga nadhiri zao za kwanza ni Sista Agatha Anord Kazonde kutoka Jimbo la Sumbawanga, Anitha Samson Nyangi kutoka Jimbo la Sumbawanga, Angela Adger Ernest kutoka Jimbo la Bukoba, Ester Robert kutoka Jimbo la Shinyanga, Getruda Robert Msiba kutoka Jimbo la Kahama, Joyce Sigela kutoka Jimbo la Sumbawanga, Sabina Amos Elia kutoka Jimbo la Shinyanga, Salvina Richard Masinga kutoka Jimbo kuu la Dodoma na Salome Stanslaus Sweya kutoka Jimbo la Shinyanga.
Wengine ni Salome Audax Lazaro kutoka Jimbo la Kigoma, Sophia Justine kutoka Jimbo la Sumbawanga, Maria Casiano Sungura kutoka Jimbo la Sumbawanga, Theresia Hamala Kija kutoka Jimbo la Shinyanga na Eunice Tuna kutoka Jimbo la Shinyanga.
Waliorudia nadhiri ni Sista Victoria Martine Msangawale ambaye ni mzaliwa wa Jimbo la Sumbawanga, Magreth Michael Lubuva mzaliwa wa Jimbo la Kondoa, Judith Deus Masumbuko ambaye ni mzaliwa wa Jimbo la Sumbawanga, Restuta Cosmas Zengo mzaliwa wa Jimbo la Shinyanga, Veronica Daudi mzaliwa wa Jimbo la Shinyanga na Tekla William Masunga ambaye pia ni mzaliwa Jimbo la Shinyanga.
Shirika la watawa wa kike la Kijimbo la Maria Mtakatifu Mama wa Huruma lilianzishwa na Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu zaidi ya miaka 5 iliyopita, ambapo kwa sasa liko chini ya ulezi wa Shirika la Maria Malkia wa mitume-Mbeya

Masista wakielekea chumba cha Ekaristia kujiandaa na adhimisho la Misa



Watumikiaji wakiongoza maandamano kuelekea Kanisani kwenye adhimisho la Misa

Masista wakiwa kwenye maandamano kuingia Kanisani kwenye adhimisho la Misa

Waanakwaya wakiwa kwenye maandamano kuingia Kanisani kwenye adhimisho la Misa

Mapare wakiwa kwenye maandamano kuingia Kanisani kwenye adhimisho la Misa

Askofu Sangu wakiwa kwenye maandamano kuingia Kanisani kwenye adhimisho la Misa

Masista wakiwa kanisani kwenye adhimisho la Misa

Bw. Projestus Silvester akisoma somo la kwanza

Bi. Winfrida John akisoma somo la pili

Wanakwaya wakiimba wakati wa adhimisho la Misa

Wanakwaya wakiwa tayari kusikiliza somo takatifu la Injili

Paroko wa Parokia ya Bukundi Padre Emmanuel Gembuya akisoma somo la Injili takatifu


Askofu Sangu akitoa mahubiri wakati wa adhimisho la Misa

Mapadre wakiwa kwenye adhimisho la Misa

Waamini wakiwa kwenye adhimisho la Misa wakati wa mahubiri



Wanovisi wa Shirika la Maria Mama wa Huruma wakiwa kwenye adhimisho la Misa kabla ya kufunga nadhiri nadhiri zao za kwanza



Wanovisi wa shirika la Maria Mama wa Huruma Jimbo la Shinyanga wakielekea mbele ya Askofu Sangu pamoja na Mkuu wa Shirika la Maria Malkia wa mitume Mbeya Sr. Christina Mwasanga, ambaye shirika lake linalilea shirika la Maria Mtakatifu Mama wa Huruma kwa ajili ya Ibada ya kufunga nadhiri zao za kwanza

Askofu Sangu akiwa na Mlezi mkuu wa shirika la Kijimbo la Maria Mtakatifu mama wa Huruma Sr. Christina Mwasanga katiba ibada ya kufunga nadhiri za kwanza

Askofu Sangu akiwahoji wanovisi juu ya nia yao muda mfupi kabla ya kufunga nadhiri zao za kwanza za maisha ya kitawa katika shirika la Maria Mtakatifu Mama wa Huruma Jimbo la Shinyanga pamoja na kuwapokea

Askofu Sangu akiongoza sala ya kubariki mavazi ya kitawa



Askofu Sangu akiwakabidhi Wanovisi Mavazi mapya ya kitawa baada ya kuyabariki















Wanovisi wakiwa wamebeba Mavazi ya kitawa waliyokabidhiwa kabla ya kufunga nadhiri zao za kwanza

Wanovisi wakirudi Kanisani kuendelea na Ibada ya kufunga nadhiri baada ya kuvaa mavazi ya kitawa waliyokabidhiwa

Wanakwaya wakiimba wimbo maalum wa wito wakati wanovisi wakiingia Kanisani

Wanovisi wakiingia eneo la Ibada ya kufunga nadhiri zao baada ya kuvaa mavazi mapya ya kitawa

Ibada ya nadhiri ikiendelea

Askofu Sangu kwa kushirikiana na Mlezi Mkuu Sister Christina Mwasanga akiwavalisha Misalaba wanavosi ambayo ni sehemu ya Mavazi rasmi ya kitawa








Wanovisi wakiwa wameshikilia mikononi viapo vyao kabla ya kufunga nadhiri zao za kwanza (wenye ua jekundu kifuani ni watawa tayari ambao wanarudia nadhiri zao kadiri ya Katiba ya Shirika la Maria Mtakatifu Mama wa Huruma -Shinyanga)

Wanovisi wakifunga nadhiri zao za kwanza za maisha ya kitawa katika Shirika la Maria Mama wa Huruma mbele ya Mungu, Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus T.K.Sangu na pamoja na Mlezi mkuu wa shirika Sr. Christina Mwasanga wa shirika la Maria Malkia wa Mitume-Mbeya










Masista wakiimba wimbo wa kumshukuru Mungu baada ya kufunga nadhiri zao



Askofu Sangu akiwapongeza Masista baada ya kufunga nadhiri zao

WATAWA na Waamini wakiwapongeza Masista wapya baada ya kufunga nadhiri zao za kwanza na wengine kurudia nadhiri



Masista wakiwa kweney Picha ya pamoja mara baada ya kupongezwa

Masista wpya wakiwa wamekaa kwenye nafasi zao baada ya Iabada ya kufunga nadhiri

Askofu Sangu akiwakomunisha Masista wapya








Askofu Sangu akiwakomunisha walelewa wa shirika la Kijimbo la Maria Mama wa Huruma





Katibu wa Askofu Padre Paul Mahona ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Ndembezi akimkaribisha Askofu Sangu kwa neno mara baada ya Misa ya nadhiri

Masista (6) waliorudia nadhiri wakiwa kwenye adhimidho la Misa

Askofu Sangu akiwakabidhi Masista wapya waliofunga nadhiri kwa mlezi wa shirika la Kijimbo la Maria Mtakatifu mama wa Huruma Sr. Christina Mwasanga wa shirika la Maria Malkia wa Mitume Mbeya


Askofu Sangu akitoa baraka kwa waamini baada ya adhimisho la Misa


Mafrateli wakiwa kwenye adhimisho la Misa

Masista wapya wakiwa mbele kwa ajili ya kupongezwa na zawadi kutoka makundi mbalimbali ya watu


Mlezi mkuu wa shirika la Kijimbo la Maria Mtakatifu mama wa Huruma Sr. Christina Mwasanga wa shirika la Maria Malkia wa Mitume Mbeya akitoa neno mara baada ya Misa ya nadhiri

Askofu Sangu akiwapongeza Masista walioweka nadhiri na kuwatakia kheri ya mwaka mpya 2024

Askofu Sangu akiwa kwenye picha ya pamoja na Masista wapya walioweka nadhiri, Mlezi mkuu wa shirika la Kijimbo la Maria Mtakatifu mama wa Huruma Sr. Christina Mwasanga wa shirika la Maria Malkia wa Mitume Mbeya

Askofu Sangu akiwa kwenye picha ya pamoja na Masista wapya walioweka nadhiri,Masista waliorudia nadhiri zao (wenye mataji ya Bluu) Mlezi mkuu wa shirika la Kijimbo la Maria Mtakatifu mama wa Huruma Sr. Christina Mwasanga wa shirika la Maria Malkia wa Mitume Mbeya

Masista wapya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu Sangu pamoja na WATAWA kutoka mashirika mbalimbali wanaofanya utume katika Jimbo la Shinyanga

Masista wapya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu pamoja na wazazi wao

Masista wapya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu Sangu na Wanakwaya


Maandamano kutoka Kanisani mara baada ya Misa

Masista wapya wakiwa kwenye maandamano kutoka Kanisani mara baada ya Misa ya kufunga nadhiri
Post a Comment