Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina
Mndeme amewasisitiza wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga, wakurugenzi,
wenyeviti wa Halmashauri maafisa elimu Mkoa wa Shinyanga pamoja na watendaji mbalimbali
wa serikali Mkoani humo kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia hali ya wanafunzi
kuripoti shuleni hasa wanaotakiwa kuanza kidato cha kwanza Mwaka huu 2024.
“Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa Mwaka 2022/2023 ilitupatia fedha za ujenzi wa madarasa kwa shule za
msingi na sekondari Mkoa umepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 53 na Milioni 687
katika sekta ya elimu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa elfu 1933, mabweni 19,
matundu ya vyoo 11elfu na 205, maabala 57, ununuzi wa madawati elfu 15,500,
viti na meza elfu 26,500, ujenzi wa nyumba za walimu mpya 69 na pia fedha
hii imeweza kugharamia elimu bila malipo”.amesema RC Mndeme.
“Natumia
fursa hii kutoa wito kwa wakuu wa Wilaya, wenyeviti wa Halmashauri, wakurugenzi
wa Halmashauri, afisa elimu wa Mkoa, maafisa elimu wa Halmashauri na watendaji
wengine wote wa serikali kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na
kidato cha kwanza Mwaka 2024 wanaripoti na kuanza masomo katika shule
walizopangiwa asiachwe hata mtoto mmoja nyuma tuhakikishe kila mtoto anapata
haki yake ya elimu”.amesema RC Mndeme.
“Ninafahamu
ufaulu wa Mwaka huu 2024 umeongezeka hivyo tunaratajia kuwa na idadi kubwa ya
wanafunzi watakaoripoti shuleni nitoe rai kwa wakuu wa Wilaya, wenyeviti wa
Halmashauri, wakurugenzi wa Halmashauri, afisa elimu wa Mkoa, maafisa elimu wa
Halmashauri na watendaji wengine wote wa serikali kuhakikisha wanafunzi wote
wanakaa kwenye madawati, kwenye viti na wanatumia meza upungufu utakaotokea
tukabiliane nao kuuondoa na nitapenda kupata taarifa ya utekelezaji wa agizo
hili kabla ya Januari 25,2024”.amesema RC Mndeme
Aidha mkuu wa Mkoa wa Shinyanga hivi
karibuni katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) alisema takribani watoto 141,000 Mkoani Shinyanga wataanza elimu ya awali na darasa la kwanza Mwaka wa
masomo 2024.
Amesema hadi Disemba 30,2023 Watoto
walioandikishwa kuanza elimu ya awali na Darasa la kwanza walikuwa 99,310 sawa na asilimia 70% ya wanaotarajiwa
kuandikishwa ambao ni 141,471
RC Mndeme amesema ujenzi wa shule za
msingi kupitia maradi wa BOOST na shule za sekondari kupitia maradi wa SEQUP
imekamilika na kusajiliwa pamoja na kupangiwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga
na kidato cha kwanza kwa mwaka 2024.
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Shinyanga
wamepongeza juhudi za serikali kuweka mazingira wezeshi kwa watoto kuanza msomo
hivyo wamewataka wazazi na walezi wenye watoto kutumia vema fursa hiyo.
Wameeleza umuhimu wa elimu ya awali na
Msingi kwa watoto ambapo wamesema ni lazima kwa wazazi na walezi kuwapa haki hiyo ya
msingi.
MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2023
Post a Comment