" BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA RASMI, MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ATOA MAAGIZO

BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA RASMI, MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ATOA MAAGIZO

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewasisitiza wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga, wakurugenzi, wenyeviti wa Halmashauri maafisa elimu Mkoa wa Shinyanga pamoja na watendaji mbalimbali wa serikali Mkoani humo kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia hali ya wanafunzi kuripoti shuleni hasa wanaotakiwa kuanza kidato cha kwanza Mwaka huu 2024.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mwaka 2022/2023 ilitupatia fedha za ujenzi wa madarasa kwa shule za msingi na sekondari Mkoa umepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 53 na Milioni 687 katika sekta ya elimu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa elfu 1933, mabweni 19, matundu ya vyoo 11elfu na 205, maabala 57, ununuzi wa madawati elfu 15,500, viti na meza elfu 26,500, ujenzi wa nyumba za walimu mpya 69 na pia fedha hii imeweza kugharamia elimu bila malipo”.amesema RC Mndeme.

Natumia fursa hii kutoa wito kwa wakuu wa Wilaya, wenyeviti wa Halmashauri, wakurugenzi wa Halmashauri, afisa elimu wa Mkoa, maafisa elimu wa Halmashauri na watendaji wengine wote wa serikali kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Mwaka 2024 wanaripoti na kuanza masomo katika shule walizopangiwa asiachwe hata mtoto mmoja nyuma tuhakikishe kila mtoto anapata haki yake ya elimu”.amesema RC Mndeme.

“Ninafahamu ufaulu wa Mwaka huu 2024 umeongezeka hivyo tunaratajia kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi watakaoripoti shuleni nitoe rai kwa wakuu wa Wilaya, wenyeviti wa Halmashauri, wakurugenzi wa Halmashauri, afisa elimu wa Mkoa, maafisa elimu wa Halmashauri na watendaji wengine wote wa serikali kuhakikisha wanafunzi wote wanakaa kwenye madawati, kwenye viti na wanatumia meza upungufu utakaotokea tukabiliane nao kuuondoa na nitapenda kupata taarifa ya utekelezaji wa agizo hili kabla ya Januari 25,2024”.amesema RC Mndeme

Aidha mkuu wa Mkoa wa Shinyanga hivi karibuni katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) alisema takribani watoto 141,000 Mkoani Shinyanga  wataanza  elimu ya awali na darasa la kwanza Mwaka wa masomo 2024.

Amesema hadi Disemba 30,2023 Watoto walioandikishwa kuanza elimu ya awali na Darasa la kwanza  walikuwa  99,310 sawa na asilimia 70% ya wanaotarajiwa kuandikishwa ambao ni 141,471

RC Mndeme amesema ujenzi wa shule za msingi kupitia maradi wa BOOST na shule za sekondari kupitia maradi wa SEQUP imekamilika na kusajiliwa pamoja na kupangiwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2024.

Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wamepongeza juhudi za serikali kuweka mazingira wezeshi kwa watoto kuanza msomo hivyo wamewataka wazazi na walezi wenye watoto kutumia vema fursa hiyo.

Wameeleza umuhimu wa elimu ya awali na Msingi kwa watoto ambapo wamesema ni lazima  kwa wazazi na walezi kuwapa haki hiyo ya msingi.

TAZAMA HAPA MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2023 NA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2023 YAMETANGAZWA.

MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2023

Post a Comment

Previous Post Next Post