" CHADEMA JIMBO LA SHINYANGA MJINI VIONGOZI MBALIMBALI WACHAGULIWA, HAMIS NGUNILA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI JIMBO

CHADEMA JIMBO LA SHINYANGA MJINI VIONGOZI MBALIMBALI WACHAGULIWA, HAMIS NGUNILA ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI JIMBO

Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini Hamis Ngunila akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.

Na Mapuli Misalaba

Wajumbe wa mkutano mkuu chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) jimbo la Shinyanga mjini  wamemchagua Hamis Ngunila kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini.

Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo Bwana Hussein Khaji amemtangaza Hamis Ngunila kuwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini.

Uchaguzi huo umefanyika leo Jumatano Januari 17,2024 katika ukumbi wa Katemi Hotel ambapo wagombea wa nafasi hiyo walikuwa watatu na kwamba kati ya kura 146 Hamis Ngunila amepata kura 110.

Wagombea wengine wa nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini ni Hassan Hamis ambaye amepata kura 30 pamoja na Asanteley Nsela amepata kura 6.

“Wenyeviti waliokuwa wanagombea jimbo walikuwa watatu wa kwanza ni Hamis Ngunila wa pili ni Asanteley Nsela na wa tatu ni Hassan Hamis hivyo sasa Asanteley amepata kuwa 6 sawaswa na asilimia 4.1, Hassan Hamis amepata kuwa 30 sawa na asilimia 20.5 na Hamis Ngunila amepata kura 110 sawa na asilimia 75.3 hivyo Hamis Ngunila namtangaza kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini”.amesema Msimamizi wa uchaguzi Khaji.

Katika kura za maoni nafasi ya katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga mjini wagombea walikuwa wawili ambapo Sebastiun Polepole amepata kura 89 sawa na asilimia 60.9 huku Joseph Ndatala akipata kura 57 sawa na asilimia 39.0.

Katika mkutano huo pia  viongozi katika nafasi mbalimbali wamechaguliwa wakiwemo viongozi wa Baraza la vijana wa CHADEMA (BAVICHA), Baraza la wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), Baraza la wazee wa CHADEMA (BAZECHA), mjumbe wa mkutano mkuu pamoja na katibu mwenezi wa CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini.

Aidha viongozi na wanachama wa CHADEMA wamewapongeza viongozi walioshinda katika nafasi mbalimbali huku wakiwasisitiza kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuzingatia taratibu za chama hicho.

Akizungumza Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini Hamis Ngunila ameahidi kufanya kazi kwa kujitoa ikiwa lengo ni kuimarisha chama ili kufikia malengo.

Msimamizi wa uchaguzi huo Bwana Hussein Khaji akitangaza matokeo.Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini Hamis Ngunila akizungumza baada ya kutangazwa mshindi katika nafasi hiyo.Katibu wa CHADEMA kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami akizungumza kwenye mkutano huo. Mwenyekiti kamati ya mafunzo CHADEMA kanda ya Serengeti akizungumza kwenye mkutano huo.Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Agatha Mamuya akizungumza kwenye mkutano huo.Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Maswa Magharibi Peter Augustino Lyamo akiwapongeza viongozi waliochaguliwa.Awali wajumbe wa mkutano mkuu wakijiandaa na zoezi la kupiga kura.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post