Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini Hamis Ngunila akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.
Na Mapuli Misalaba
Wajumbe wa mkutano mkuu chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA) jimbo la Shinyanga mjini wamemchagua Hamis Ngunila kuwa Mwenyekiti wa
CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini.
Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi
huo Bwana Hussein Khaji amemtangaza Hamis Ngunila kuwa mshindi wa nafasi ya
Mwenyekiti CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini.
Uchaguzi huo umefanyika leo Jumatano
Januari 17,2024 katika ukumbi wa Katemi Hotel ambapo wagombea wa nafasi hiyo
walikuwa watatu na kwamba kati ya kura 146 Hamis Ngunila amepata kura 110.
Wagombea wengine wa nafasi ya Mwenyekiti
wa CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini ni Hassan Hamis ambaye amepata kura 30
pamoja na Asanteley Nsela amepata kura 6.
“Wenyeviti
waliokuwa wanagombea jimbo walikuwa watatu wa kwanza ni Hamis Ngunila wa pili
ni Asanteley Nsela na wa tatu ni Hassan Hamis hivyo sasa Asanteley amepata kuwa
6 sawaswa na asilimia 4.1, Hassan Hamis amepata kuwa 30 sawa na asilimia 20.5 na
Hamis Ngunila amepata kura 110 sawa na asilimia 75.3 hivyo Hamis Ngunila
namtangaza kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA jimbo la
Shinyanga mjini”.amesema Msimamizi wa
uchaguzi Khaji.
Katika kura za maoni nafasi ya katibu wa
CHADEMA Jimbo la Shinyanga mjini wagombea walikuwa wawili ambapo Sebastiun
Polepole amepata kura 89 sawa na asilimia 60.9 huku Joseph Ndatala akipata kura
57 sawa na asilimia 39.0.
Katika mkutano huo pia viongozi katika nafasi mbalimbali
wamechaguliwa wakiwemo viongozi wa Baraza la vijana wa CHADEMA (BAVICHA),
Baraza la wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), Baraza la wazee wa CHADEMA (BAZECHA),
mjumbe wa mkutano mkuu pamoja na katibu mwenezi wa CHADEMA jimbo la Shinyanga
mjini.
Aidha viongozi na wanachama wa CHADEMA
wamewapongeza viongozi walioshinda katika nafasi mbalimbali huku wakiwasisitiza
kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuzingatia taratibu za chama hicho.
Akizungumza Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la
Shinyanga mjini Hamis Ngunila ameahidi kufanya kazi kwa kujitoa ikiwa lengo ni kuimarisha
chama ili kufikia malengo.
Msimamizi wa uchaguzi huo Bwana Hussein Khaji akitangaza matokeo.
Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini Hamis Ngunila akizungumza baada ya kutangazwa mshindi katika nafasi hiyo.
Katibu wa CHADEMA kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti kamati ya mafunzo CHADEMA kanda ya Serengeti akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Agatha Mamuya akizungumza kwenye mkutano huo.
Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Maswa Magharibi Peter Augustino Lyamo akiwapongeza viongozi waliochaguliwa.
Awali wajumbe wa mkutano mkuu wakijiandaa na zoezi la kupiga kura.
Post a Comment