" CHADEMA WILAYA YA SHINYANGA MJINI KESHO KUFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI NAFASI MBALIMBALI ZA JIMBO

CHADEMA WILAYA YA SHINYANGA MJINI KESHO KUFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI NAFASI MBALIMBALI ZA JIMBO

TAZAMA VIDEO HII

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Shinyanga mjini,  kesho kitafanya uchaguzi wa viongozi wa nafasi mbalimbali ngazi ya jimbo na mabaraza ya chama.

Nafasi zitakazogombewa ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti, katibu, katibu wa siasa na uenezi, pamoja na viongozi wa mabaraza ya chama hicho.

Akitoa taarifa hiyo msimamizi wa uchaguzi jimbo la Shinyanga mjini Charles Bullet amesema uchaguzi huo umetanguliwa na zoezi la usaili wa wagombea katika nafasi hizo za jimbo.

Kwa upande wake katibu wa CHADEMA Wilaya ya Shinyanga Bwana Joseph Ndatala amewaomba wagombea kuendelea kuzingatia miiko na maadili ya katiba ya CHADEMA huku akiwaomba wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post