Mwenyekiti wa chama cha ACT
Wazalendo Mkoa wa Shinyanga Chrisant Joseph Msipi akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.Na Mapuli Kitina Misalaba
Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga wamemchagua Chrisant Joseph Msipi kuwa Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga kwa kipindi cha Miaka mitano ijayo.
Uchaguzi huo umefanyika leo Alhamis Januari 18,2024 katika ukumbi wa mikutano Katemi Hotel na kwamba umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hichi akiwemo Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Taifa Mhe. Dorothy Semi.
Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo Bwana Mbarala Maharagande amesema wagombea wa nafasi hiyo walikuwa watatu ambapo amemtangaza Chrisant Msipi kuwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga akiongoza kwa kura 19 kati ya kura 35.
Wagombea wengine waliogombea nafasi hiyo ni Said Juma amepata kura 13 huku Merchiory Sebastian akipata kura 3.
“Nafasi ya Mwenyekiti wa ACT Wazalendo iligombewa na watu watatu ndugu Merchiory Sebastian amepata kura tatu (3), ndugu Said Juma amepata kura kumi na tatu (13) na Chrisant Msipi amepata kura 19 kwa mamlaka ya usimamizi wenu wa Mkoa wa Shinyanga namtangaza rasmi ndugu Chrisant Msipi kuwa ndiyo Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga”.amesema msimamizi wa uchaguzi Maharagande
Msimamizi wa uchaguzi huo amemtangaza Omary Gindu kuwa mshindi wa nafasi ya katibu wa chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Shinyanga ambapo kati ya kura 38 Omary Gindu amepata kura 20 huku Bi. Sili Yasin Swedi akipata kura 18.
Aidha katika mkutano huo safu ya viongozi katika nafasi mbalimbali imechaguliwa akiwemo katibu habari uenezi, mahusiano na umma mwekahazina, katibu mipango na chaguzi, mwenyekiti ngome ya wazee, mwenyekiti ngome ya wanawake, mwenyekiti ngome ya vijana, katibu ngome ya wazee, katibu ngome ya wanawake, katibu ngome ya vijana, wajumbe wawili wa kamati ya uongozi (wanaume) pamoja na wajumbe wawili wa kamati ya uongozi (wanawake).
msimamizi wa uchaguzi
huo Bwana Mbarala Maharagande akitangaza matokeo ya uchaguzi wa viongozi nafasi mbalimbali.
Mwenyekiti wa chama cha ACT
Wazalendo Mkoa wa Shinyanga Chrisant Joseph Msipi akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.
Msimamizi wa uchaguzi huo, katibu wa idara wa haki za binadamu na makundi maalum Taifa ambaye pia ni Waziri kivuli katiba na sheria Mbarala Maharagande akizungumza kwenye mkutano.
Post a Comment