Na Mapuli Kitina Misalaba
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga nimefanya misako na kukamata vitu na vielelezo mbalimbali wakiwemo watuhumiwa 76 wa makosa ya wizi, Bunduki moja, pamoja na vipande 120 vya Nondo.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari, kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amesema jeshi hilo limefanya doria na misako takribani Mwezi mmoja kuanzia Disemba 21 Mwaka 2023 hadi Januari 23 Mwaka huu 2024.
Kamanda Magomi ametaja vitu na vielelezo vilivyokamatwa ikiwemo Mafuta ya Diseli lita mia moja, Pikipiki, Bangi kilo mbili na kete kumi pamoja na vifaa mbalimbali vya kupigia ramli chonganishi.
“Katika doria na misako iliyofanyika tumefanikiwa kukamata Bunduki moja(1) aina ya Shortgun Pump Action yenye namba za usajili MV. 95738V ambayo iliibiwa huko katika kijiji Mondo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga pia tumekamata Simu mbili (2), Mafuta ya Diseli lita mia moja(100), Pikipiki nane(8), Betri tatu(3) za Gari, Kompyuta mpakato (Laptop) mbili (2), EMS Foot messager moja(1), Redio moja(1) na Spika moja(1)”.
“Vitu vingine tulivyokamata ni vipande 120 vya Nondo, Mifuko 4 ya Unga wa Ngano, Mafuta ya kula lita 15, vipande nane vya Bomba, vipande tisa vya Vyuma(angle line), Mashine mbili za kusukuma Maji, Exterision cable moja, Grader moja, Sigara pakiti 30, Pombe ya Moshi lita 105, Mirungi bunda 94, Boksi tano za vifaa tiba aina ya Gloves, Goroli 125 za kusaga Mawe, mtambo mmoja wa kutengeneza Pombe ya Moshi, Sufuria moja, Bhangi kilo mbili na kete kumi pamoja na vifaa mbalimbali vya kupigia ramli chonganishi ambapo tumekamata watuhumiwa 76 katika vituo mbalimbali”.amesema Kamanda Magomi
Kwa upande wa Mahakama Magomi amesema jumla ya kesi 11, zim epata mafanikio zikiwemo kesi mbili za kubaka ambapo washtakiwa wamehukumiwa Miaka 30 jela, wizi wa mifugo pamoja na shambulio la kudhuru mwili.
“kesi mbili za kubaka ambapo washtakiwa wamehukumiwa Miaka 30 jela, kesi moja ya wizi wa Mifugo washtakiwa wawili walihukumiwa Miaka miwili jela, kesi moja ya kujeruhi mshtakiwa mmoja alihukumiwa Mwaka mmoja kifungo cha nje jela, kesi moja ya wizi mshtakiwa alihukumiwa miezi tisa jela, shambulio la kudhuru Mwili, kesi tatu washtakiwa watatu walihukumiwa miezi mitatu jela, kesi mbili washatakiwa wawili walihukumiwa kwenda jela kati ya miezi mitatu hadi sita na kuingia kwa jinai kesi moja mshtakiwa alihukumiwa kwenda jela miezi mitatu”.amesema Kamanda Magomi
Wakati huohuo kamanda Magomi amesema jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kitengo cha usalama barabarani limekamata jumla ya makosa 4846 ambapo makosa 4844 watuhumiwa wamewajibishwa kwa kulipa faini za papo kwa papo huku wengine wakifikishwa Mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi ya kisheria.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amewashukuru wananchi kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kupambana na uhalifu na wahalifu kwa kutoa taarifa huku kamanda huyo akiwataka madereva na watembea kwa miguu kutii na kuheshimu alama, michoro na sheria za usalama barabarani wakati wote wanapokuwa Barabarani.
Post a Comment