Kampuni
ya JK Wall Puty Africa Limited imeendesha mafunzo kwa mafundi ujenzi na
wauzaji wa vifaa vya ujenzi wa mkoa wa Mwanza ili kuwajengea uwezo na
kuongeza ufanisi katika kazi zao za kila siku wanazozifanya
Akizungumza
katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Rock City Mall jijini Mwanza
mgeni rasmi ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias
Masala akimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe CPA Amos Makala mbali
na kuipongeza kampuni hiyo kwa kazi nzuri inazozifanya pamoja na kutaka
kuharakishwa kwa utekelezaji wa mpango wa kampuni hiyo wa kujenga
kiwanda cha kuchakata malighafi na kutengeneza bidhaa za Saruji nyeupe
nchini badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi
'..
Niwasisitize katika kile mlichokisema juu ya kuanzisha kiwanda nchini
kwaajili ya uchakataji wa malighafi na kutengeneza bidhaa hapa hapa
nchini tofauti na awali ambapo mlikuwa mnaingiza bidhaa moja kwa moja
nchini kutoka nje ..' Alisema
Aidha
Mhe Masala amezisifu bidhaa za JK Wall Putty kwa namna zilivyo bora,
kupatikana kwa urahisi sokoni, gharama nafuu na kupendwa na watumiaji
walio wengi huku akizitaka kampuni nyengine kuiga mfano wa kampuni hiyo
kwa kuwajali wateja wake na kurejesha sehemu ya faida kwao
Nae
meneja wa mauzo na masoko wa kampuni ya JK Wall Putty African LTD Kwa
Kanda ya Ziwa Ndugu Michael Malili mbali na kuelezea ubora wa bidhaa zao
kwa watumiaji ameongeza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo
watumiaji wa bidhaa zao pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili ili
kuongeza tija katika kazi zao
Kwa
upande wake meneja wa mauzo na masoko kutoka Kanda ya Kati Ndugu Albert
Kingu amewaasa mafundi ujenzi kuendelea kutumia bidhaa za kampuni yake
ya kwamba ni nzuri, bora, zina gharama nafuu na kupatikana kwa urahisi
Paul
Mtatiro ni fundi kutoka kata ya Igoma na Zaituni Nasibu ni fundi
mwanamke kutoka kata ya Igogo kwa pamoja wameshukuru kutolewa Kwa
mafunzo hayo na kwamba yamewajengea uwezo katika kazi zao watakazokuwa
wakizifanya Kila siku na kuomba utaratibu huo uwe endelevu Ili kutatua
kero na changamoto wanazokutana nazo sanjari na kuwashauri mafundi
wenzao kuzingatia kilichofundishwa
Kampuni ya JK Wall Putty Africa Limited pia imetoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake mara baada ya kuisha Kwa mafunzo hayo.
Post a Comment