
Wanafunzi wa shule ya msingi Mwamalasa iliyopo kata ya Magalata wilaya ya Kishapu na Mkoani Shinyanga wametakiwa kutokupokea zawadi kwa watu wasiowafahamu ili waepukane na kufanyiwa ukatili wanapokuwa njiani, shuleni, mtaani na nyumbani.
Rai hiyo ilitolewa Januari 26, 2024 na Mkaguzi Kata wa Kata ya Magalata Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Charles Chacha alipotembelea shule hapo kwa dhana la ushirikishwaji jamii ili kutokomeza uhalifu na wahalifu.
Mkaguzi Chacha alitoa Elimu juu ya madhara ya kupokea zawadi kwa watu wasiowafahamu ambazo usababisha kufanyiwa ukatili na kukatisha ndoto za masomo yao.
Vile vile Mkaguzi Chacha alihitimisha kwa kusema utii wa Sheria na kufuata taratibu za shule ikiwa ni pamoja na kuwatii Walimu na Wazazi wao kwani nidhamu ndiyo msingi wa mafanikio.
Kutoka Dawati la Habari Polisi Mkoa wa Shinyanga
Post a Comment