" MAHAFALI YA 7 WAHITIMU 59 CHUO KIKUU HURIA TAWI LA SHINYANGA, DIWANI MHE. MKWIZU AKUMBUSHA KUJIENDELEZA NA ELIMUA YA JUU.

MAHAFALI YA 7 WAHITIMU 59 CHUO KIKUU HURIA TAWI LA SHINYANGA, DIWANI MHE. MKWIZU AKUMBUSHA KUJIENDELEZA NA ELIMUA YA JUU.



Na Mapuli Misalaba
Jumla ya wanafunzi  59, wamehitimu katika chuo kikuu Huria cha Tanzania Tawi la Shinyanga huku wakiwaomba watanzania kujiendeleza na elimu ya juu ili kuwa na Taifa bora la watu wasomi.

Sherehe hiyo imefanyika katika ukumbi wa Katemi Hoteli na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ambapo mgeni rasmi ni Diwani wa kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Mhe. Victor Mkwizu.

Akizungumza Diwani huyo wa Ngokolo Mhe. Victor Mkwizu ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wanafunzi hao kwa kuhitimu masomo hayo salama huku akiwapongeza walimu kwa ufaulu mzuri unaoonekana katika chuo kikuu Huria tawi la Shinyanga.

Diwani Mhe. Mkwizu amewaomba wakazi wa Manispaa ya Shinyanga hasa wenye elimu ya chini kuchukua hatua za kujiendeleza na elimu ya juu ili kuongeza wigo wa uelewa katika maisha ya kila siku.

Aidha Mhe. Mkwizu ameahidi kuendelea kushirikiana na chuo hicho ikiwemo kuzifikisha sehemu husika changamoto zinazowakabili ili kufikia malengo yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo kikuu Huria tawi la Shinyanga  Dkt. Agatha Mgogo amesema mahafali hayo niya saba (7) tangu kuanzishwa kwa chuo hicho tawi la Shinyanga na kwamba kati ya wahitimu 59, wanawake 35 na wanaume 24.

Dkt. Agatha Mgogo amewaomba wakazi wa Mkoa wa Shinyanga na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kujiunga na chuo hicho ili kupata elimu ya aina mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti hadi PHD.

Baadhi ya wahitimu waliohudhuria kwenye sherehe hiyo wamewaomba watanzania kutoridhika na elimu ya chini huku wakiwahimiza kujiendeleza na elimu ya juu ili kuwa na Taifa bora la watu wasomi.

Chuo kikuu Huria ni chuo kikuu cha umma kinachotoa mafunzo katika vitu mbalimbali ikiwemo Elimu, Biashara, Sayansi ya Mazingira pamoja na Sheria kwa usomaji wa masafa.


Baadhi ya wahitimu katika chuo kikuu Huria tawi la Shinyanga wakiwa kwenye mahafali.


Diwani wa kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Mhe. Victor Mkwizu akizungumza kwenye mahafali hayo.




Rais wa chuo kikuu Huria tawi la Shinyanga Esther Aron kagurumjuli akizungumza kwenye sherehe hiyo.



Diwani wa kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Mhe. Victor Mkwizu akiwa katika zoezi la kukabidhi vyeti kwa wahitimu.

Mkurugenzi wa chuo kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga Dr. Agatha Mgogo akizungumza kwenye mahafali hayo.



Rais wa chuo kikuu Huria tawi la Shinyanga Esther Aron kagurumjuli akisoma lisala katika mahafali hayo.

Post a Comment

Previous Post Next Post