Na Mapuli Misalaba
Mazishi ya Msichana Joyce Hezron John mwenye umri wa Miaka
14 Mkazi wa Mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, ambaye pia
alikuwa ni Mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya sekondari Mazinge katika
Manispaa ya Shinyanga yamefanyika katika makabuli ya Dodoma kata ya Ndembezi
Manispaa ya Shinyanga.
Marehemu Joyce alizaliwa Februari 5, 2009 Babati Mkoani Manyara
ambapo elimu ya msingi alisoma na kuhitimu 2021 katika shule ya msingi Bugoyi B
iliyopo Manispaa ya Shinyanga.
Mwaka 2022 alijiunga kidato cha kwanza shule ya sekondari
Mazinge iliyopo Manispaa ya Shinyanga na kwamba amefariki Mwaka huu 2024 akiwa
kidato cha tatu.
Marehemu Joyce Hezron alifariki Jumamosi majira ya saa tatu
usiku Januari 13,2024.
Aidha Mchungaji wa Kanisa la AICT Kambarage Charles Lugembe
wakati akihubiri kwenye ibada fupi ya kumwombea marehemu Joyce Hezron ambayo
imefanyika nyumbani alipokuwa anaishi, ametumia nafasi hiyo kuitaka jamii
kutafuta hekima inayosaidia kujua namna ya kuishi nyakati katika maisha ya kila
siku.
Mchungaji Lugembe amewakumbusha watanzania kuendelea kuishi
maisha ya kumpendeza mwenyezi Mungu huku akisisitiza kuacha tabia za kupuuza mafundisho ya viongozi
wa Dini.
Pia amesema katika kuishi maisha ya Duniani ni vyema kila mtu kuwa
na utaratibu wa kufikiria maamuzi sahihi na siyo kufanya maamuzi mabaya ambayo
hayampendezi Mungu ambapo amehimiza kujiepusha na mambo mabaya.
Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota
ameshiriki ibada ya kumwombea marehemu Joyce Hezron ambapo ibada hiyo
imehudhuriwa na viongozi mbalimbali, jamii na wadau wakiwemo viongozi wa
kampeni ya kupinga ukatili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga.
Zoezi la kuaga mwili wa marehemu Joyce Hezren likiendelea.
Post a Comment