Tazama wanachama wapya wa CCM kata ya Kitangili wakiapa.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Bwana Mussa Ngangala amewaapisha wanachama wapya 131 baada ya kujiunga na chama hicho katika kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.
Uapisho huo umefanyika Jumatano Januari 24,2024 kwenye mkutano wa ndani wa chama hicho kata ya Kitangili ambao umekwenda sanjari na maadhimisho ya CCM kutimiza Miaka 47 ifikapo Februari 5 Mwaka huu 2024.
Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mussa Ngangala ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewaapisha wanachama wapya 131 ambao wamejiunga na chama hicho kutoka kwenye matawi ya CCM kata ya Kitangili ikiwemo tawi la Imalilo, Kitangili, Iwelyangula, Songambele pamoja na tawi la Sokoine.
Ngangala amewapongeza wanachama hao wapya kwa kujiunga na chama hicho huku akiwaomba kuendelea kushirikiana ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na viongozi waliopo madarakani kwa lengo la kuchochea uchumi wa Taifa.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mussa Ngangala ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi anaoshirikiana nao, kwa kuimarisha usalama wa nchi ambapo amewaomba watanzania kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita hasa kwenye shughuli za maendeleo.
Ametoa rai kwa wanachama wa CCM kata ya Kitangili kuendelea kupendana, kushirikiana na kuwu na tabia ya uvumilivu, kuepuka utengano huku akisisitiza kuwa na kipaumbele zaidi katika masuala ya maendeleo ili kufikia malengo waliojiwekea.
Pia amezungumzia suala la mmomonyoko wa maadili ambapo amewaomba wazazi, walezi na jamii kuendelea kuwafundisha watoto maadili mema ili waweze kukua katika misingi mizuri ya Taifa la Tanzania.
Wakati huo huo amewakumbusha viongozi wa CCM kata ya Kitangili kuendelea kuongeza wanachama wapya ikiwa ni pamoja kusajiri kwa njia ya kielekroniki huku akiwahimiza kujiandaa na uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa Mwaka huu.
Aidha awali katibu CCM kata ya Kitangili Bwana Deus Numbi wakati akisoma taarifa ya ujenzi wa ofisi ya CCM kata hiyo amesema zipo changamoto mbalimbali zilizokwamisha kuendelea kwa ujenzi huo ambapo amemuomba mgeni rasmi kusaidia ikiwemo Mchanga, Nondo, mbao za kufunga lenta pamoja na mpira wa kumwagilia.
Akizungumzia ujenzi wa ofisi hiyo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mussa Ngangala ameahidi kutoa vifaa vyote ambavyo vimekwamisha ujenzi huo ikiwemo Mchanga, Nondo na Mbao ambapo pia ameiomba kamati ya ujenzi kuandaa bajeti ya mahitaji yote ili aweze kutekeleza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kitangili Mhe. Mariam Nyangaka amesema hali ya usalama katika kata hiyo ni usalama na kwamba zaidi ya Bilioni tatu zimetukika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya elimu, Afya pamoja na barabara.
Diwani wa kata ya Kitangili Mhe. Mariam Nyangaka akimpokea mgeni rasmi, mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mussa Ngangala baada ya kuwasili kwenye mkutano huo.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mussa Ngangala akipokelewa baada ya kuwasili kwenye mkutano huo.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mussa Ngangala akimkabidhi kati cha CCM mmoja wa wanachama wapya.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mussa Ngangala akimkabidhi kati cha CCM mmoja wa wanachama wapya.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mussa Ngangala akimkabidhi kati cha CCM mmoja wa wanachama wapya.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha
mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mussa Ngangala akimkabidhi kati cha CCM mmoja
wa wanachama wapya.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mussa Ngangala akiwaapisha wanachama wampya 131 wa CCM kata ya Kitangili.
Wanachama kutoka kwenye matawi mbalimbali ya Kita ya Kitangili wakiwa kwenye mkutano huo wa ndani.
Tazama wanachama wapya wa CCM kata ya Kitangili wakiapa.
Post a Comment