Na Mapuli Misalaba
Serikali Mkoani Shinyanga imefanikiwa kumrejesha
shule binti mkazi wa kijiji cha Iyugi kata ya Lyamidati Halmashauri ya Wilaya
ya Shinyanga ambaye aliolewa baada ya kufaulu kuingia kidato cha kwanza Mwaka
huu 2024.
Hayo yamebainishwa na mkuuwa Mkoa wa Shinyanga Mhe.
Christina Mndeme wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema,
mwanafunzi huyo alipata ufaulu wa wastani wa A katika mtihani wake wa kumaliza
darasa la saba.
Mwanafunzi huyo aliozeshwa baada ya kumaliza darasa
la saba ambapo familia ile inasemekana kuchukua mahari ya jumla ya Ng’ombe 15
na kumruhusu binti huyo kwenda kuanzisha maisha ya ndoa ambapo serikali
imefanikiwa kumrejesha shule mpaka sasa anaendelea na masomo.
“Katika
hali ya kusikitisha baadhi ya wazazi badala ya kuwapeleka shule watoto
wanawaozesha tukio hili limetokea Mkoani Shinyanga katika kata ya Lyamidati
kijiji cha Iyugi mzazi mmoja mtoto wake amefaulu vizuri sana kwa wastani wa A
Mzazi huyo aliamua kumuozesha mtoto wake kwa kupokea mahari ya Ng’ombe 15”.
“Nawashukuru sana wananchi waliotupatia
taarifa hiyo takini pia nawashukuru viongozi pamoja na jeshi la polisi kwa kuhakikisha
kwanza mtoto huyu anaondolewa kwenye Ndoa na kuja kuendelea na masomo yake
shuleni”.
“Na
huyu mzazi aliyeozesha mtoto amekimbia tunaendelea kumsaka popote alipo
tumfikishe katika vyombo vya sheria na niwaombe wanaume acheni kuoa wanafunzi
waacheni wapate haki yao”. amesema RC Mndeme
Post a Comment