Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Magadula Humphrey Mtafungwa akizungumza na Misalaba Media
Msichana Joyce Hezron anayekadiriwa kuwa na Miaka 17 Mkazi wa Mtaa wa Magadula kata ya Ngokolo
Manispaa ya Shinyanga, ambaye pia ni Mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya
sekondari Mazinge katika Manispaa ya Shinyanga amefariki Dunia kwa kile
kinachosadikiwa kuwa kifo chake kimetokana na kunywa sumu
Kwa Mujibu wa Watu walioshuhudia tukio hilo wameeleza kuwa
chanzo cha kifo chake kimetokana na kunywa sumu,baada ya kugombezwa na Babu
yake, akituhumiwa kutumia fedha iliyotumwa
kwenye simu yake kwa bahati mbaya.
Wameeleza kuwa kabla ya kifo chake Msichana huyo alipokea
mwamala wa fedha kiasi cha shilingi elfu sitini,ambayo ilitakiwa kutumwa kwa Bibi
yake lakini kwa bahati mbaya ikaingia kwake na kwamba aliitumia kwa matumizi binafsi bila idhini ya wakubwa
Misalaba Media,imezungumza na Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Magadula
Humphrey Mtafungwa ambaye amekiri kuwa na taarifa za kifo cha msichana huyo mkazi wa mtaa wake,ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba
wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao ili kuwaelekeza zaidi kuhusu mambo
yanayofaa na yasiyofaa.
“Asubuhi kwenye saa mbili na nusu nilipigiwa simu na balozi akinitaarifu kuwa katika mtaa wangu kuna msiba umetokea usiku wa jana saa nne, nilipofika kwenye eneo la tukio niliongea na familia wakanieleza kweli msiba umetokea na alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Mazinge sekondari mpaka sasa hivi taratibu za maziko zinaendelea tunatarajia kuhifadhi mwili siku ya Jumanne”.amesema Mwenyekiti Mtafungwa
Post a Comment